SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Reviewing Wedding Guest’s Looks At Raya & Barnaba’s Wedding
Mitindo

Reviewing Wedding Guest’s Looks At Raya & Barnaba’s Wedding 

Watu maarufu mbalimbali walihudhuria katika reception ya mwanamuziki Barnaba na mkewe Raya ambao wamefunga ndoa week iliyopita, well tupo hapa kureview nani alivaa nini na was it giving what it suppose to give au its a failed assignment?

Nandy Na Billnas tunaweza kusema hii ni favorite look yetu of the night, color cordination, fit zimewakaa vyema, stylish, neatly done hair styles & makeup, tumependa kwamba Nandy amevaa nguo ndefu lakini yet ameonyesha some skin kupitia sheer zilizopo pembeni ya gauni. They did that japo kwa Nandy kifuani kidogo ilitaka kuharibu but tunaweza kusamehe.

Suit @jm_international_collection
Dress @nellsoamtee

Wema Sepetu & Whozu, Wema alipendeza na hii yellow dress, tumependa kwamba ameachia nywele lakini mbele zimebanwa vyema kuonyesha makeup na hereni lakini pia kuacha nguo ionekane vyema, the design tumeshaiona mara nyingi kwake we need something new, Whozu alivaa red suit haikuwa mbaya sana kila mmoja akikaa kivyake lakini pamoja imetupa feeling ya vidonge vya amoxicillin all in all wakikaa tofauti tofauti walipendeza.

Suit by @jm_international_collection

Dress by @designed_by_shuu

Hamisa Mobetto alipendeza na gauni yake tunadhanii hii style ya kuvaa gaunifupi then chini ina sheer fabric ndio trend kwasasa, unajua ile unataka kushow off lakini kama hutaki kushow off skin ndio hii, tumependa that ametumia color nyeusi chini imefanya the look kuonekana putted together, makeup na nywele on point.

Dress- @mobettostyles
Mua- @makeupbyjojotz
Hair stylist- @certified_perucaz

Gigy Money alivalia long velvet dress yenye sheer pembeni look ilikuwa nzuri decent hajaonyesha too much skin, lakini ingekua vyema zaidi kama nywele zingenyanyuka since gauni inashingo ndefu kidogo na imefunikwa sehemu nyingi,lakini pia the bag was a miss kwetu.

Hair @luluzhair
Makeup @gigy_money_og
Pochi @vbs_royaltrends
Picha @chizimapicha

Linah Sanga, alivalia short dress ambayo ilikuwa ni off shoulder, idea ya hii dress haikuwa mbaya lakini piece ya juu na chini haviingiliani yaani ni kama vitambaa vilibaki na hawakujua waviweke wapi wakaingizia tu kwenye hii gauni, tunadhani wangetumia fabric moja juu na chini ingependeza zaidi.

Esma Platnumz, tumeona better than this kwa Esma, kwetu tunadhani angeweza kufanya vyema zaidi, vazi tumeshaliona mara nyingi kwa wengine so kuliona kwake ilikuwa afanye zaidi ya wengine lakini imekuwa kawaida, pia viatu alivyovaa na hili vazi haviingiliani, kama unavaa vazi linafika mpaka chini the least unaweza kufanya ni kuvaa open sandals ilikuonyesha skin lakini pia kupata kimo kidogo.Nyele na makeup on point.

Lace @esma_dangote
Fundi @asbahdesign
Makeup @nonoglams
Nywele @certified_perucaz
picha @barty_photographer

Anyways Afromates tupe maoni yako, look ya nani umeipenda zaidi?

Related posts