SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Sababu 4 Zinazoharibu Style Yako
Mitindo

Sababu 4 Zinazoharibu Style Yako 

Inawezekana unapenda kuonekana stylish, unapenda kuvaa mavazi yanayovutia na kukufanya uonekane unaenda na mitindo, unanunua mavazi mazuri ya gharama lakini bado huoni kama unafanikiwa kufikia lengo lako, hii hutokea kwa kila mmoja wetu na sio wewe peke yako na hutokana na sababu hizi 4.

  • Mawazo

Mawazo hu-play part kubwa sana katika mitindo, inawezekana unajaribu sana kiasi kwamba una haribu au haujiamini kwamba style yako uliyoichagua inakufaa na kuendana na wewe. Hii hutokana na wengi wetu kudhani style ni kuvaa mavazi yanayo-trend kwahio chochote unachokiona kipo kwenye trend unaenda nacho mwishoe unanunua vitu vingi ambavyo una-doubt navyo ukivivaa na kukukosesha confidence.

  • Fit

Hata ukiwa na mavazi mazuri au brand kubwa kiasi gani kama haziku-fit vyema basi hakika lazima style yako iharibike, hakikisha unaponunua mavazi yanakuwa size yako, hayapungui sana wala kukubana sana bali ni size yako inayokutosha kama zikizidi incase utanenepa basi hakikisha zinakuachia kidogo sana.

  • Kutokujua Style Yako

Kutokujua personal style yako ni tatizo kubwa pia, unatakiwa kujua nini upo comfortable nacho na kipi haupo comfortable nacho. Lakini pia rangi gani unaona unavaa mara nyingi na zipi huzikuvutii, body type yako ina ruhusu aina zipi za mavazi? ukijua vyote hivi na mavazi yako kukutosha sawia basi muonekano wako utabadilika.

  • Shoe Game Weak

Viatu ni game changer linapokuja katika swala la mavazi, unaweza ukavaa simple lakini ukaongeza na statement shoe na muonekano wako ukabadilika kabisa kutoka boring to boujiee, lakini pia vinaweza kuporomosha muonekano wako mzima unaweza kuvaa mavazi mazuri ukavaa na kiatu cha hovyo basi hapohapo muonekano wako ukaharibika kabisa.

hakikisha una pair chache za viatu zinazoingia katika mavazi ya aina tofauti tofauti lakini pia quality ya hivyo viatu ni nzuri na vinaendana na style yako.

Related posts