Kwenye maswala ya mavazi katika top 10 essential clothes kuwanazo lazima utakutana na highwaist trouser hizi zina play part kubwa sana katika mitoko ya sehemu mbalimbali iwe official, casual au kwenye occasion yoyote inategemea na unavyo style kutokana na uendapo, well sahau kuhusu high waist trouser zinazo kiki kwa sasa ni hizi suruali ambazo zinavaliwa kifuani
peek of the day-One Shoulder Top x High Waist Pants by Style Pantry
Mara ya kwanza tulimuona nayo mwanamitindo kutoka South Africa Lelizwe Sibisi akiwa amevalia hii beige chest trouser kutoka kwa @StylealertSA, hii suruali inakaa kama off shoulder jumpsuit kwa hio hakuhitaji shirt kwa juu amevaa yenyewe tu kama ilivyo, ame add some glamour kwa kuvaa statement dropped earrings na kichwani alikuwa na wave hair,love it anaweza kwenda brunch au movie date na hii outfit.
Tv Personality kutoka South Africa K Naomi Noinyane yeye alivaa suruali kutoka kwa hao hao StylealertSA, ya rangi hio hio ya beige, yeye aliamua iwe casual kwa kuvaa suruali hii na kicks huku akimalizia muonekano wake na bucket hat na saa. “comfortability at it best”
Tumemuona mwenyewe mbunifu wa hii suruali StylealertSA akiwa ameivalia in chic way ambapo alistyle na statement gold earrings, block heels huku akiwa amemalizia na nude makeup na pixie cut hair style.
Kwetu tulimuona fundi cherehani wa kishua Jacqueline Wolper yeye amejaribu kushona ya kwake tofauti kidogo, yake ameshona kama bwanga na aliamua kuivalia na kimono cha kitenge alicho match na kiremba kichwani akamalizia na hoop earrings na heels. Tumependa kwamba Jacqueline amejaribu ku-dare.
Well tuambie would you try this trend or nah?
Related posts
2 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/sahau-kuhusu-high-waist-trouser-sasa-hivi-tunavaa-suruali-kifuani/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/sahau-kuhusu-high-waist-trouser-sasa-hivi-tunavaa-suruali-kifuani/ […]