SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Si Lazima Kuvaa Rangi Za Brand Siku Unapopewa U-ambassador
Mitindo

Si Lazima Kuvaa Rangi Za Brand Siku Unapopewa U-ambassador 

Its about time watu maarufu wanatumika kuwa brand ambassador kwa makampuni mbalimbali, kwetu sisi hii ni habari njema kwamba ma-kampuni wanatumia watu kutoka nyumbani kutangaza bidhaa zao.

Tumeona watu maarufu mbalimbali wakichukua deals hizi kama Diamond Platnumz, Gigy Money, Nandy pamoja na Harmonize. Well kwetu sisi hii ni habari njema, lakini asilimia kubwa ya hawa wasanii wametushangaza na mavazi yao wakati wanaenda kutangaza kwamba wamekuwa brand ambassadors wa kampuni hizo.

Wengi wao wameonekana kuvalia mavazi yanayo endana na rangi za brand hizo, kitu ambacho kimetufanya tuwaze je ni moja kati ya makubaliano yao na hizo kampuni au ni wao wanaona vyema waka-match na rangi ya brand hizo? Well si mbaya inaonyesha commitment yako na brand hio lakini Je hayo mavazi au hizo rangi zinavaliwa sawia?

Wengi wao tumeona wanachukulia tu poa mavazi yao kwenye hili lakini ni moja ya vitu ambavyo jamii huwa ina notice sana.

Kama ni brands huwa zinataka watu maarufu wavalie rangi ambazo zinaendana na brand zao basi ni vyema watu hawa maarufu wakatafuta stylist ambao wanajua kupangilia mavazi na rangi. Hii itaepusha aibu hizi ndogondogo kwa sababu tunaamini huwa wanaambiwa tarehe fulani kuna hili na hili kwahio wanakuwa na muda wa kujiandaa.

Lakini kama ni watu maarufu wenyewe basi wajue si lazima kuvalia rangi za brand kuna rangi nyingi ambazo ni neutral unaweza kuvaa bila kuleta conflict of interest Kama

  • Nyeupe
  • Nyeusi
  • Nude
  • Gray

Bado ukawa umevalia vyema na bila kupoteza deal yako. Lakini pia tuangalie na mavazi gani yanatakiwa kuvaliwa katika event kama hizi, hii ni business kwaio si mbaya sana kama ukatafuta suit au something nice kuonekana profesional hata kama unavaa rangi za kampuni hio.

Related posts

3 Comments

  1. Buy DMT Vape pen for Sale Victoria

    … [Trackback]

    […] Read More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/si-lazima-kuvaa-rangi-za-brand-siku-unapopewa-u-ambassador/ […]

  2. Asbestos Abatement Norco

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/si-lazima-kuvaa-rangi-za-brand-siku-unapopewa-u-ambassador/ […]

  3. click the up coming website page

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/si-lazima-kuvaa-rangi-za-brand-siku-unapopewa-u-ambassador/ […]

Comments are closed.