SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Sinema Zetu International Film Festival 2018
Mitindo

Sinema Zetu International Film Festival 2018 

Weekend ndefu ya pasaka imeisha na tume enjoy kwa namna moja au nyingine, lakini katika weekend hii kulikua na mengi makubwa likiwepo la Sinema Zetu Film Festival. Ambapo tamasha hili lilifanyika Tarehe 1, 2018 ni Tamasha la kwanza na linahusiana na kutoa Tuzo za filamu hii inawahusu wote wanao husiana na utengenezaji na uigizaji wa Filamu.

Wasanii mbalimbali walikuwepo kama Wema Sepetu, Gabo Gozimba, Chuchu Hansy na wengine wengi, kama kawaida sisi jicho letu lilikuwa katika red carpet kuona nani kavaa nini katika Tamasha hili. Well Ooh Well kwetu tulitegemea vingi sana hasa kutokana na sisi hivi kuna fashion pages nyingi mno Tanzania, wengi tukijaribu kutoa Tips na kukosoa pale panapo kuwa wrong, tunaweza kusema kwa kiasi fulani tunaelekea tunapo taka japokuwa bado hatujafika.

Sisi tulitegemea kupata WOW factors lakini tofauti ni kwamba wengi walikuwa vile ambavyo tumewazoea, tumesha mzoea fulani na dress code ya aina fulani basi ndio hiyohiyo aliyo ivaa katika Sinema Zetu Film Festival lakini si mbaya sana japo tungependa pia kungekuwa na daring

Lavie Makeup in Elisha Red Label Dress – Lavie alivaa gauni jeusi kutoka kwa mbunifu Elisha ambalo lilimtosha vizuri kabisa, Theme ya event ilikuwa mavazi ya kistaarabu ambayo aliendana nayo vizuri the dress was very elegant

Hamisa Mobetto na yeye aliattend hii event akiwa amevalia gauni kutoka kwa Elisha Red Label, seems like Elisha ametamba sana katika hii event, well the dress was nice simple & elegant, Imeonyesha her curves very well japo nywele hazikutuvutia kivile lakini Hamisa ameingia katika Best Dressed wetu wa siku hii.

Faiza Ally tunaweza kusema kama tutamuona Faiza mara nyingi katika hizi event anaweza kuingia katika fashion icons wa red carpet anajua kujipatia, this dress was so fine japo kifuani kama ime pwaya but she did a good job katika kuchagua vazi ameendana na theme her make up is so finey.

Wema Sepetu nae alivaa gauni kutoka kwa Elisha Red Label na yeye alivaa a black dress ambayo ilikuwa kama na turtle neck, amemaliza muonekano wake na blonde bob, tumependa ame add some color kwenye hili vazi kwa kuweka nywele za rangi japo tungependa zaidi kama nywele zingebanwa ili tuone vizuri uso wake.

Shilole hatuwezi kusema ameingia kwenye best dressed au kwenye worse alikuwa vuguvugu ila kutokana na historia yake ya kuwa na mavazi ya ajabu tunaweza kusema amejitaidi hapa.

Ommy Dimpoz akiwa amevalia suit kutoka kwa mbunifu jm_international_collection na yeye ameingia katika list yetu ya walio pendeza japo he could have done better with the shoes.

Worse Dressed

Chuchu Hansy well theme ya event ilikua ni sinema zetu, za kwetu sisi na wala sio Indian’s chuchu didn’t get the memo

Diamond sio mbaya na wala sio nzuri japo tulitagemea more kutoka kwake, that blazer is fire ila suruali na viatu vime haribu muonekano we loved the upper him ila the rest is not working to us.

Mboni Masimba this was a Film Festival na wala sio ulienda pale kuangalia movie, ametu-disappoint kwa kweli too casual for the event.

Makeke & his team tunajua kwamba hii ni festival ya sinema zetu, utamaduni una ruhusiwa kuhusika ila hii ilikuwa too much, tunajua kama wewe ni mbunifu na ungependa kuona tamaduni zetu zinaendelezwa tunadhani ungeweza kubadilisha huu muonekano na kuwa modest na cultural kwa wakati mmoja ili kupata something nice, hatujui mliwezaje kukaa na wenzenu na hizo nyungo too much is harmful sometimes.

Well hayo ni mawazo yetu sisi tuambie wewe kwako unadhani nani alipaswa kuwa wapi?

Related posts

4 Comments

  1. DMT for sale Perth

    … [Trackback]

    […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/sinema-zetu-international-film-festival-2018/ […]

  2. Christensen arms

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/sinema-zetu-international-film-festival-2018/ […]

Comments are closed.