Ramadhani ndio kwanza inaanza, Najua wengine ni kama mimi, tunawaza mabibui yenyewe machache nilio nayo na yanipasa nivae Stara kila siku nikiwa ofisini, Najua fika kwamba wote tunapenda kuonekana wapya kila siku ndio maana leo nikaamua kuandaa makala hii juu ya Maxi Sketi, Zipo za Rangi mbalimbali inategemea na mvaaji mapenzi yake.

Maxi sketi ni sketi ndefu zinazo ishia kabla ya kikonyo cha mguu, sketi hizi ni nyepesi zinaachia (hazibani) na zipo kimitindo Zaidi. Ukizivaa hazikupi shida unakua huru kwa sababu hazibani unaweza kuruka ata mtaro na pia haina shida ya kuzishikilia kusema ni ndefu sana.
Maxi SketiKitu kizuri kuhusu maxi sketi unaweza kuzivaa kwa kuzilinganisha na rangi za hijab kwa namna mbalimbali na pia una weza kuzi vaa na viatu vifupi,virefu,ndala na hata makobazi.
Maxi sketi inaweza kuvaliwa popote, kazini, kwenye matembezi na hata kwenye sherehe na marafiki.

JINCHI YA KUIVAA MAXI SKETI NA VITU VINGINE

Unaweza kuvaa kwa kuchanganya rangi tofauti tofauti ila ziendane na muekano
Unaweza kufananisha maxi sketi na mtandio wako ukaonekana maridadi na umejihifadhi (stara)

Maxi Sketi ImevaliwaPia unaweza Kuvaa Kizibao na kuchanganya rangi tofauti touti ili kuleta muonekano mzuri,wa kisasa na ukawa bado umejistiri maungo yako vizuri.