Hivi vipochi unaweza kuwa umekutana navyo mahala mbalimbali, wamama wanauza sana na kuvitengeneza mno mitaani, wengi huwa tunavipuuzia na kuvipita lakini brand kutoka hapahapa Tanzania iitwayo So Rare wao wameviona na kuvipa muonekano wa tofauti kidogo.

Kwa sababu vinauzwa sana na wamama basi wengi tunahisi vinabebwa na wamama wa umri fulani wao wameviweka katika hali ya usichana na kutuonyesha namna hata mdada anaweza kuvibeba.

Well wanatengeneza wenyewe na hizi clutch na hii ilikuwa look book ya collection ya spring summer 2018 wamezipa clutch hizi jina la “TALLY CLUTCH”

Tumependa jinsi walivyo jitaidi kutoa locality katika photo-shoot yao na the fact that wamefikiria kufanya photo shoot kwa ajili ya clutch hizi, ni kitu cha tofauti na kinahitaji kusifiwa inaitwa “branding” ndio maana unaweza kukuta mbunifu anauza plain tee kama wewe ila tu sababu logo ni gucci ikachukuliwa Gucci.

Kama ungependa kununua au kupitia kuona bidhaa zao nyingine clich hapa @SoRare