Kama tunavyojua kwenye kila kitu kuna essentials needs hivyo kwenye workout na gym basi kuna baadhi ya vitu hautakiwi kukosa kuwa navyo. Unaambiwa gym and workouts essentials zimegawanyika katika sehemu sana ila leo tungependa kudeal na baadhi ya vitu ambavyo ni dhambi kubwa sana kukosa kuwa navyo wakati ukiwa gym au wakati unafanya workouts.
Ningependa kuzigawa essentials hizi kwa makundi tofauti tofauti, ila kwa siku ya leo tungeanza na workout and gym clothes. Hakuna kitu kizuri kama kuwa na gym au work out clothes na ni moja ya essentials kubwa sana, ningependa kukuonyesha essential clothes hizo kama ifuatavyo;
Workout au gym clothes : ni moja ya essentials muhimu sana kwa sababu mtu hawezi akafanya mazoezi na nguo za kutokea yaani uvae nguo kama vile gauni ukiwa gym lazima utaonekana wa ajabu sana hivyo kwenye workouts na gym clothes vinainclude vitu vifuatavyo.
1. Sneakers
Hauwezi kwenda gym au unado workouts na heels, ballet flats au sandals, unatakiwa uvae sneakers ambayo itaku-fit na iwe nzuri. Unaweza ukavaa nike runners kwa ajili ya mazoezi na ni viatu ambavyo ni vyepesi sana.

Vaa sneakers ambazo unajua zimetengenezwa kwa ajili ya mazoezi kwa sababu vitakufanya uwe na muonekano mzuri na utakuwa comfortable ukiwa unafanya mazoezi. Usisahau kuwa sneakers nzuri katika mazoezi inaongeza morale ya kufanya mazoezi to the maximum.
2. Tops and bottoms
Vaa vitu ambavyo vitakufanya uwe comfortable na kukufanya usmile hauwezi kuvaa shirt ya ofisini gym, au vazi ambalo halitokufanya uwe comfortable na usmile muda wote kulingana na maumbile ya mwili wako.

Kwenye swala la top na bottoms consider sana kuhusu kitambaa cha hivyo vitu hauwezi ukaenda na tshirt au tracksuits ambayo sio kwa ajili ya workouts kwa hiyo considers sana aina ya materials za nguo zako. Hakikisha zinakufit vyema na zina stretch vyema kama tunavyojua Gym kuna hekaheka ukivaa nguo haikutoshi inaweza ikachanika au ikawa nzito na kukuzuia kufanya kilichokupeleka kwa uzuri.
3.underthingies
Underwear, sports bras, socks ni vitu muhimu sana katika kupata great workout outfit. Hauwezi kwenda mazoezin au gym ukiwa umekosa kuwa na hivi vitu kwani ni muhimu sana kwa sababu tofauti tofauti kwa mfano sport bras kwa wanawake ni muhimu sana kwa sababu mwanamke anaweza akawa anafanya mazoezi ya kujump ili aweze kufeel comfortable na workout au gym session basi ni vizuri avae sport bras kwa.

Pia socks na underwear ni vitu muhimu kwa sababu inasaidia kucover eneo ambalo halitakiwi kuonekana muda wa gym au workouts.
Note: hii ni part one ya essentials things ambazo ni muhimu sana katika gym na workouts kwa upande kwa clothes kati ya hivi vitu ni kitu gani ambacho wewe hauwezi kuskip kuvaa wakati unaenda gym au unafanya workouts. Asante kwa mda wako part 2 inakuja sio mda mrefu.
Imeandikwa na @gotchathegreatest
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…