SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Style Mpya Za Jokate Zawashtua Mashabiki
Mitindo

Style Mpya Za Jokate Zawashtua Mashabiki 

Jokate Urban Mwegelo, wengi tunamjua kama kidoti au Jojo, Jokate ni moja kati ya watu maarufu walio tikisa sana kwa upande wa mitindo na wengi tulikuwa tunamuangalia kama inspiration yetu, well over the years style ya Jokate imebadilika mno, na tumepata maoni mengi kuhusu mionekano yake kadhaa huku wengi wakituuliza imekuwaje?

Hizi ni 2 cents zetu kutokana na mabadiliko ya style za Jokate

Kazi Mpya

Wengi tulikuwa tunamjua Jokate kama Miss, Mwanamitindo, Muimbaji, Muigizaji na sasa Jokate yupo kwenye kitengo kingine kabisa ambacho kina muhitaji kuwa na mavazi decent, tulizoea kumuona na vimini, jeans lakini sasa hivi tunamuona na suits etc na ni lazima tuone amebadilika, japo pia Jokate anahitaji kunyanyua mionekano yake kidogo hata kama ni kitengo kipya basi suit zake ziwe stylish.

Umbo Jipya

Jokate wa zamani alikuwa na mwili mdogo ambao ulikuwa una mruhusu kuvaa karibia kila aina ya mavazi, lakini kwasasa Jokate ame gain mwili kwa kiasi chake, lazima style zake zitabadilika kutoka sehemu moja kwenda nyingine tunachokiona kwake ni kwamba bado hajaukubali huu mwili mpya anajaribu kuuficha.

Kuwa Mama

Ofcourse zamani Jokate hakuwa na majukumu makubwa alikuwa na muda wa kujiangalia mwenyewe, lakini kwasasa anamajukumu ana kazi na ana mtoto inawezekana hapati muda wa kujiangalia kikamilifu, kulea si lele mama,

Je Jokate anatakiwa kufanyaje kwenye hii situation?

  • Ajikubali.
  • Let Go- aondoe ambavyo havimfai kwasasa
  • Ajue Style Yake Anyoitaka Kwasasa
  • Afanye Manunuzi Mapya

Tunadhani tumpe muda wa yeye kujipata (lol)

Namna Ya Ku-style Mavazi Baada Ya Mabadiliko Ya Mwili

Related posts