Tuna long weekend inakuja, sikukuu ya Maulid Ya Mtume kwa ndugu zetu waislam imeangukia Ijumaa tunapumzika siku 3, kwa wale ambao tuna mialiko na hatujui tuvae nini hapa ni mahala pako, umealika watu na hujui uvae nini karibu hapa na huna mualiko ila tu unataka kuvaa upendeze hatuja kusahau karibu pia.
Kwetu Tanzania tukialikwa Maulid basi tunachojua moja kwa moja kuvaa ni dera au baibui hata kama mtu hana atafanya juu chini alipate lakini kumbe kuna mavazi mengine yapo kabatini kwako unaweza kuchukua ukayavaa
Kwa sasa wengi wetu tuna long vimono/shirt dress unaweza ukawa nayo kwenye kabati yako unavaaga kwa juu au yenyewe, unaweza kuivaa kama dress ndani ukavalia na skin tight ndefu kwa ndani, unaweza kuvaa na flat shoes au heels, funga mtandio vizuri na hakikisha umepangilia rangi vizuri.
Maxi Skirt, these are a must have. Kila mwanadada ana paswa kuwa nazo unaweza kuvaa maxi skirt yako uliyo nayo na shirt au blouse, usisahau kufunika nywele na unaweza ku accessorize mtoko wako na miwani,hereni au chochote upendacho.
Maxi dress nayo pia ni vizuri kuwa nayo kama unayo kabatini kwako unaweza kuivaa kwenye maulid gathering jua tu namna ya kuibadilisha kutoka kwenye normal maxi dress to a gathering maxi dress, accessorize, vaa heels your good to go
Stylish Abaya
hopeful tumekusaidia nini kesho uvae wakati unaenda kwenye mualiko wako,
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/stylish-outfit-for-maulid-day-gathering/ […]