Kila tunapopata muda tunajaribu kutathmini tasnia yetu ya mitindo Tanzania inape elekea. Kwa sasa tunadhani tunaenda pazuri ukiangalia wabunifu wengi wanajaribu ku-push katika ubunifu na kuonekana wa tofauti, tukiangalia Duniani wenzetu wanajaribu sana kuumiza vichwa kuwa creative na design zao. Wanajaribu wao ndio wawe wa kwanza kuonyesha design fulani hata kama kuna mwingine atafanya lakini tunajua original ali debut mbunifu fulani.
Lakini pia tukiongelea Tasnia ya mitindo kwa ujumla sio tu wabunifu lakini kuna models na makeup artist pia, ambao tunaweza kusema nao wanajitahidi kulingana na uwezo wao. Japo ni wachache mno ambao wapo creative na kazi zao.
Tumekuwa tukiona nyuso zilezile katika majukwaa,wabunifu walewale, make up artist walewale, models wale wale, mwisho wa siku unaenda katika fashion event unajua kabisa collection ya mbunifu fulani mwanamitindo fulani atakuwepa na katika collection yake hapata kosa aina hii ya vazi na makeup artist atakuwa fulani mwisho wa siku tuna go around the same cycle haturudi nyuma wala kwenda mbele.
Sisi tunadhani tunahitaji sura mpya katika hizi kazi ziwe beauty pageant, iwe fashion show, ziwe red carpet tunahitaji watu ambao wata tutambulisha vitu vipya, tukiangalia kwa wenzetu kila siku wabunifu wapya wana tambulishwa kila siku makeup artist mpya ana kuja na wapo very creative na hii inatokana na mtu kupenda anachofanya na sio kukifanya kwa sababu anahisi anaweza na kuingia pesa.
Kwetu tuna mfano wa makeup artist mzuri tu Grace Malikita au Cherie Mals ukiingia katika account yake utakuta vitu vya tofauti, ni moja kati ya makeup artist ambae sisi tunahisi akipewa nafasi ya kufanya kitu kama kupaka makeup’s za models katika fashion show tutapata kitu cha tofauti, ukiangalia katika fashion show za wenzetu mbunifu ana weka umakini katika kila kitu makeup ya models zake ziweje, mpangilio atatafuta stylist ampangie mpangilio wa mavazi ili kuonekana tofauti. Kwetu utaona same makeup na hair style kuanzia mwanzo wa show mpaka mwisho it’s become real boring.
Kuna clothing line ambazo zina chipukia nazo tunahisi zikipewa nafasi zitafanya mapinduzi makubwa kama sio ku-debut collection yao katika fashion show’s kubwa basi hata wapewe nafasi ya kufanya collaboration na wabunifu wakubwa kuna vintaged.lads hawa huwa wana tengeneza jeans wana spice up jeans kwa kuongezea michoro na vitu tofauti tofauti hicho ambacho tunacho kitaka creativeness, tunahisi kama wakipewa nafasi ya kufanya kitu na mbunifu mmoja hapa Tanzania tunaweza kupata kitu cha tofauti.
lakini pia wapo styleyoursoul.clothing ambao wao wana fanya ubunifu wa nguo lakini za kwao ni more advanced yaani kitu ambacho unaweza kununua na kuuza kama retail, tunadhani hawa pia wakipewa mkono tunaweza kupata kitu cha tofauti kutoka kwao as tumezoea kuona vitenge na khanga majukwaani tukiwapa nafasi na watu ambao wana fanya vitu vingine kwa utafauti ili kuwapa nafasi wale wengine ambao wanahisi hawana cha kuona zaidi ya vitenge na khanga waje waone vitu vingine.
Tunahitaji creativity na ili kuipata ni lazima tupate fresh people ambao wana fresh ideas za tofauti, mara kwa mara tunaona watu wapya wanaibuka na kupewa attention lakini mwisho wa siku unaona mbona huyu anafanya kama fulani yaani kaibuka kwa sababu tu anaweza kufanya kile ambacho fulani anafanya hana jipya. Tunahitaji kuwapa nafasi watu ambao wana ideas za tofauti kitu kipya katika tasnia, tunaona jinsi ambavyo wenzetu wana wanyanyua vipaji vipya tunapata kuona watu wengine wanafanya nini cha tofauti na si kama sisi walewaliopo ndio haohao na hata akija mpya anafanya kilekile we need new creative people.
Related posts
2 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/tasnia-ya-mitindo-tanzania-inahitaji-sura-mpya/ […]
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/tasnia-ya-mitindo-tanzania-inahitaji-sura-mpya/ […]