Ooh mama Tetema, Afroswagga tetema. Well wasanii Rayvanny na Diamond Platnum wameachia video ya nyimbo yao kali, TETEMA. Stylists waliotumiwa ni Noel Ndale, Vaazi pamoja na Macrida Joseph ambao tumewaona wakistyle video nyingi za WCB.
Kila tuonapo alert ya video toka WCB tumesharidhika kukutana na crazy hair styles, accessories nyingi yaani bling bling kupitiliza pamoja na outfits zikiwa tracksuits na durags kichwani. Hupati shauku ya kuona vitu vipya kabisa
Ni katika scenes chache sana waweza bahatisha mambo mazuri kimavazi as tumeona Rayvanny na the dancers in full white looking good lakini vingine ni kila siku vitu vile vile. Ubunifu katika styling pia set up haupo. Kiufupi ukitazama waishia kutetema ukinung’unika.
Stylists watumiwapo basi huwa twategemea kuona kazi yenye upekee lakini ukimuona Rayvanny, toka nywele hadi viatu, ni the same Rayvanny kila siku alojawa na fashion mistakes hivyo huenda stylists hawatumiwi kikamilifu na na kupewa nafasi ya kumbadilisha mtu muonekano ipasavyo.
Always twalia na ubunifu katika kazi za wasanii wetu. Wasanii wana nguvu kubwa ya ushawishi kwa watu ikiwemo katika mavazi pia. Hivyo yafaa kuwa makini ili kuleta ushawishi sahihi kwa mashabiki. Hakika utatetema upitapo barabarani ukijionea vijana wengi ndani ya tracksuits, ugly daddy shoes mostly Balenciaga na offwhite, plus cheni shingoni. It’s the signature WCB style ambayo wengi wameiadopt lakini haivutii hata bali yatetemesha.
The styling walofanyiwa back up dancers, wakivalia red berets na red pants imeweza kuvutia na pia the full white dress code ya Rayvanny and Diamond’s dancers nayo imependeza. Though Zaidi ya hapa yawweza kufanyika
Lakini twatamani tukiona vitu bora zaidi toka kwa WCB. Stylists watumiwapo, wapewe nafasi ya kufanya kazi tujionee ubunifu haswa,unaweza kuangalia video hapo chini na kutupa maoni yako
Imeandikwa na @Willibard_jr
Related posts
4 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/tetema-music-video-fashion-review/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/tetema-music-video-fashion-review/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/tetema-music-video-fashion-review/ […]
… [Trackback]
[…] Here you will find 70348 more Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/tetema-music-video-fashion-review/ […]