SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

The Denim Knee High Covers Trend
Mitindo

The Denim Knee High Covers Trend 

Kama kuna kitu tunajua kwa hakika ni kwamba kila mwaka denim (jeans) lazima i-trend na kwa namna za kipekee kabisa, kulikuwa na skin jeans, zikaja mom jeans, tukaenda kwa distressed jeans, kukawa na deconstructed jeans na sasa tumehamia kwenye denim knee high covers.

Denim knee high covers hizi ni kama socks au tight ambazo zinaziba mguu mpaka kwenye goti, hizi haziji na kiatu chake yaani unaweza kuvalia kiatu chochote iwe sandals, boots, raba ni wewe tu na chaguo lako.

Tumeona watu maarufu mbalimbali kutoka Tanzania wakiwa wamevalia trend hii ambapo tumemuona Paula Kajala, Phina na Abby Chams

Well hizi covers zinafaa kuvaliwa usiku, kwenye party na zinaendana sana au kupendeza sana kama utavaa na kitu kingine cha denim juu iwe coat, skirt au pants.

Utaweza kujuliza kwanini nivae?

  • Zinakufanya uonekane tofauti (unique)
  • Kama unaenda sehemu ina baridi itakukinga na baridi
  • Kama kuna mbu na hutaki kuvaa mavazi marefu ina faa pia
  • Kama unavaa viatu ambayo hudhani kama vinaendana na vazi ni namna nzuri ya kuficha viatu hivyo
  • Kama una insecurity na miguu yako lakini ungependa kuvaa nguo fupi basi ni namna nzuri pia ya kuficha miguu.

Anyways tuambie a clap or slap kwenye hii trend?

Related posts