3) MAAMUZI SAHIHI KAMA SEKTA YA MITINDO IPO TAYARI KUKUPOKEA
Tathimini uwezo wako na utu wako vizuri kabla ya kuingia katika kazi ya ubunifu. Unaweza kupenda nguo lakini nguo ni sehemu tu ya simulizi katika kufanya ubunifu, unahitaji kua na lugha nzuri,utayari wa kufanya kazi,uwe na uwezo wa kuzimudu hisia zako ukikosolewa, uwezo wa kukubali kuwa na wateja wengi au ma bosi na kuwa na nidhamu katika kazi yako.
Kuwa mbunifu ni kazi yako endapo tu: utakubaliana kuipa hii kazi maisha yako yote, kuwe na utayari wa kusimamia unacho amini, kuwa na mawazo tofauti kuhusu mambo muhimu katika mitindo, sikiliza wateja wako vizuri, jua mitindo ya ndani na je unapo ishi kwa kifupi kula,lala na pumua ukiwa unawaza kuhusu mitindo.
Kuwa mbunifu hakuwezi kuwa kazi yako endapo: huwezi kumudu msongo wa mawazo vizuri, unataka kazi isiyo kuwa na mabonde na miteremko, unahitaji watu kusifia kazi zako na nguvu zako, unachukia kupoteza fedha zako na pia una mambo mengi una hitaji kuyafanya katika maisha.
4)JIANDAE KWA AJILI YA MAFANIKIO
Pata elimu kuhusu upande wa biashara katika mitindo: kuwa mbunifu mwenye mafanikio hakuhitaji tu kuwa na kipaji na ubunifu bali inahitaji pia elimu katika biashara ba masoko katika sekta ya mitindo. Pata taarifa za nini kinatokea katika ulimwengu wa mitindo kwa kusoma au kutembele kwenye masoko.
Jifunze Zaidi ya ubunifu: kuna ugavi unao husika katika sekta ya mitindo na unahitaji kujua kila kazi inayo husiana nayo. Jua kiundani kuhusu biashara ya mitindo fanya utafiti kipi wengine wana fanya.
Mjue mteja wako: kujua nini mteja wako ana taka na kupendelea ni kitu chenye uzito sana katika mitindo unahitaji kuwa na uwezo mkubwa wa kufahamu mteja ana taka nini ili kumfanya ajisikie huru na arudi tena siku nyingine.
Wajue washindani wako: siku zote angalia wengine wana fanya nini, halafu kifanye Zaidi yao ili kukipa muonekano tofauti
Maonyesho ya biashara: ni sehemu ya kujifunza kiundani Zaidi na kuelewa Zaidi jinsi sekta ya mitindo inavyo fanya kazi, kipi kita kusaidia ili kufikia mahitaji ya mteja na kudumu katika ushindani.
b) Tafuta kazi za ubunifu: unahitaji kuwa na uzoefu kabla ya kusimama mwenyewe hii itasaidia kukuchonga hata pale utakapo simama mwenyewe kuto kuyumbishwa, kupata kazi katika sekta ya mitindo inategemea na wewe una taka kufanya mitindo ya aina gani.
5) Jenga mtindo wako Kwingineko:Kusanya kazi zako za mitindo mfano michoro au kazi ulizo zifanya hii itasaidia kukupa soko kirahisi kwa maana uwezo wako utaonekana kupitia io michoro na itakua rahisi kwa waajiri wako au wafanyakazi wenzio kuona uwezo wako katika ubunifu
- Michoro ya mikono au picha ya kazi zako
- Michoro ya kompyuta
- Rangi au nguo katika kuwasilisha Au chochote kinacho onyesha kazi yako kwa ufasaha
Related posts
4 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/timiza-ndoto-yako-ya-kuwa-mbunifu-sehemu-ya-mwisho/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/timiza-ndoto-yako-ya-kuwa-mbunifu-sehemu-ya-mwisho/ […]
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/timiza-ndoto-yako-ya-kuwa-mbunifu-sehemu-ya-mwisho/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/timiza-ndoto-yako-ya-kuwa-mbunifu-sehemu-ya-mwisho/ […]