Vidole kutokeza nje ya kiatu hukupa muonekano mbaya, inawezekana umenunua viatu vinakutosha vyema ila ukavivaa ukiwa umepaka lotion miguuni kwenye sole viatu vikawa vinateleza au inawezekana una tatizo la jasho miguuni ambayo nayo husababisha miguu kuteleza kwenye viatu na sababisha vidole vitokeze mbele,either way tuna tip kwaajili ya kuzuia tatizo hili.
- Hair Spray
Kama unajijua una hili tatizo basi pale ambapo unataka kuvaa viatu ambavyo ni open sandals basi kwanza anza na kupulizia hair spray kwenye viatu vyako na acha mpaka ikauke ndio uvae spray husaidia kufanya miguu yako igandane na viatu na kuzuia kuteleza, yes unaweza kuvaa na kuvua tukisema kuganda usije kudhani ni kama gundi.
- Double Sided Tape
Kuna tape zile ambazo zina gundi mbele na nyuma, hizi pia zinaweza kusaidia. Bandika gundi hizi katika sole ya kiatu chako kisha vaa itafanya mguu ushindwe kusogea mbele au kurudi nyuma na utakaa vyema kwenye kiatu, hii tip aliwahi kuiongelea muigizaji Jessica Alba.
Ni matumaini yetu tips hizi zitakusaidia, tuambie je wewe huwa unafanya nini ukipatwa na tatizo hili?
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/tip-ya-kuondokana-na-vidole-kutokeza-nje-ya-kiatu/ […]