SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Tips On How To Be The Chicest Pregnant Woman At The Office
Mitindo

Tips On How To Be The Chicest Pregnant Woman At The Office 

Kama ukiwa kawaida tu huna ujauzito sometimes unapata hasira kuchagua nini uvae ofisini then tambua hali hii huwa mara mbili zaidi kwa wajawazito. Mara nyingi maofisini wajawazito huwa wanaonekana wanajitupa au mimba zimewajia vibaya (lol). Wengi huwa wanaamua kushona au kununua maguo marefu wakavaa tu ila kuna namna kama ni mpenzi wa fashion inaweza kuku-turn off kama unapenda fashion na ungependa kupendeza ofisini na una ujauzito basi hizi tips zitakusaidia.

Slip Dress

Hizi ni rahisi sana kwenye kuzivaa na zipo classy kama zinaweza kuwa na long slevee au short sleeves ukavalia na blazer au kimono juu ukapendaza

Loose Two Pieces

Kuna zile siku unajisikia kuvaa suruali, ili kuepuka zile hekaheka uvalie na top ipi basi nunua loose two pieces ambazo unaweza kuvaa pamoja na nzuri zaidi kama suruali ikiwa na elastic waist.

Black Dress

Black dress inaweza kuwa styled mara nyingi kwa namna nyingi bila ya kuwa noticed, lakini pia black inasaidia kukufanya uonekane slim so inaweza kusaidia sana kwenye kipindi cha ujauzito.

Bodycorn Dress

Unataka kushow off the bump na kujisikia sexy basi hii ni a go to, itakuchora vizuri lakini pia ina option nyingi za kuvaa unaweza kuvalia raba, heels au sandals kuifanya ionekane classy unaweza kuongezea blazer au casual kwa kuvalia denim coat

Over Sized White Shirt

Moja kati ya essentials ambazo nazo unaweza kuvaa mara nyingi, unaweza kuvaa na jeans, skirt au leggins na bado ikakupa nafasi ya kupumua na kuonekana elegant ofisini

Matenity Shirt Dresses

Hizi ni nzuri zile siku hujisikii kuwa na nguo nyingi mwilini lakini pia ni vazi ambalo unaweza kuvaa hata baada ya kujifungua

Skirts

Skirts ni moja ya mavazi ambayo yapo comfortable ukiwa na ujauzito, hasa zile zenye elastic waist, unaweza kuvalia juu ya tumbo zikakukaa vyema kabisa, ukavaa na top yako na blazer ukapendeza vizuri tu. Lakini pia kuna options mbalimbali kama pleated skirts, pencil skirts, skater skirts etc.

Well slayage njema mama Kija

Pictures By @emmalynlove_

Related posts