Kama mfanyakazi mpya ni kazi kujua namna gani uvae ofisini, lakini tu sio kama mfanyakazi mpya inawezekana upo kazini muda mrefu lakini huridhishwi na muonekano wako, unatamani kubadilisha muonekano wako lakini hujui pa kuanzia, tuna tips ambazo zinaweza kukupa muelekeo wa nini ufanye.
- Play it safe
Umeanza kazi hujui ni nini kinaendelea katika ofisi hio badala ya ku-underdress au ku-over dress jaribu ku-play it safe, nunua essentials kama black blazer, white button down shirt, calm color blouse, kama mpenzi wa suruali unaweza kununua official trouser za blue,black na nude, kama mpenzi wa skirt au magauni pia nunua ambayo unajua unaweza kuvaa mara nyingi na hazito fanya muonekano wako uwe over au underdressed.
Kama bado unatamani kujua zaidi basi jaribu vifuatavyo
- Angalia mtandaoni mavazi ya ofisini
- Angalia kwenye website unayoenda kufanya kazi
- Uliza kwa wafanyakazi au boss wa kampuni hio kama wana rules zozote
Hizi tips tatu zitasaidia kujua uvae au ununue nini kuliko ku-assume halafu ukafika huko ukaonekana kituko, kwa wale ambao tayari mmeshaanza kazi ila unataka ku-upgrade muonekano wako umeshajua ofisi inahitaji nini, jaribu kufikiri ni aina gani ya style unaitaka na uangalie mtandaoni kinacho kufaa.
- Jua aina tofauti za styles za mavazi ya ofisini
Kuna aina 3 tofauti za mavazi ya ofisini, unatakiwa kufanya research yako na kujua kipi kinakufaa zaidi, na hii hasa inatokana na mazingira ya ofisi lakini pia kuna position yako inahitaji nini, huwezi kuvaa skirt unafanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi, jaribu kujua position yako na kipi kinakufaa na jua tofauti ya
- Business formal
- Business Casual
- Smart Casual
Business formal hii ni ile ipo ki-proffessional zaidi unahitaji mavazi ambayo ni formal zaidi kuliko casual hapa unaweza kuangukia kwenye suit, gauni au formal skirts pia rangi zake ni zile ambazo zimetulia.

Business casual na Smart casual hizi kwa kiasi zinaingiliana na pia hapa ni more of relaxed outfit unaweza ku-mix casual wear na formal wear kama kuvaa jeans na button down shirt, unaweza kuvaa t-shirt na pencil skirt etc.

- Tafuta namna ya kuwa comfortable
Hakuna kitu kina kera kama kutokuwa comfortable hata kazi yako hautoiona nzuri, hakikisha chochote unachovaa upo comfortable nacho kama hujazoea kuvaa skirt basi unaweza kuvaa suruali na bado ukaonekana professional na kama hujazoea kuvaa suruali basi vaa skirt au gauni ulilozoea hakikisha tu linaendana na mazingira ya ofisi, usivae vitu vya ku-tight sana ukashindwa hata kusogea au kuvaa mavazi yasiyobana sana ukaonekana umevaa oversized.
Tukutakie week njema.
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…