SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Tips Za Namna Ya Kuvaa Ukiwa Na Matiti Makubwa
Mitindo

Tips Za Namna Ya Kuvaa Ukiwa Na Matiti Makubwa 

Linapokuja suala la kuvaa ikiwa maziwa yako ni makubwa, jambo kuu ni kupata mitindo inayopendeza figure yako.
zingatia haya kama maziwa yako ni makubwa.

  • Vaa Bra inayokutosha,

hii inasaidia na ni muhimu sana pia pimwa na mtaalamu ili kubaini ukubwa wa sidiria yako, bra ya kuunga mkono hii itainua na kutengeneza kifua chako na kuunda silhouette ya usawa zaidi.

  • Chagua vitambaa vinavyofaa.

Mfano vitambaa vinavyoning’inia vizuri kwenye mikunjo bila kujirundika, vitambaa kama chiffon au jezi vinaweza kukupendezesha. Epuka vitambaa vizito ambavyo vitajirundika kwenye kifua chako.

  • Chagua V-necklines

hizi zinaunda muonekano mzuri kuelekea chini na kurefusha kiwiliwili pia hupunguza ule muonekano wa maziwa makubwa.

  • Vaa nguo za kushona,

kama unapata tabu kununua nguo zinazokutosha vizuri jaribu kushona nguo hapa itakusaidia kupata ile size na muonekano unaotaka maana unaposhona unaamua nguo ikukae vipi tofauti na kununua.

  • Sawazisha Silhouette yako,

oanisha sehemu za juu za mwili na za chini ziwe sawa. Mfano sketi za mistari, suruali pana au jeans ya bootcut inasaidia kuunda silhouette ya uwiano zaidi.

  • Kumbuka kuvaa kitu kinachokufanya uwe comfortable na mwenye ujasiri pia,

usivae nguo inakubana sana pia usivae nguo kubwa sana itabadili muonekano wa mwili wako, let this be your starting point but personal style and preferences should always take precedence

Imeandikwa na @this_is_lydia._

Related posts