SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

TOFAUTI YA MBUNIFU,STYLIST NA FUNDI CHEREHANI
Mitindo

TOFAUTI YA MBUNIFU,STYLIST NA FUNDI CHEREHANI 

Aug 22, 2016 Tuliandika hili andiko kuhusu wabunifu, washonaji na stylist nini tofauti zao na jinsi wanavyo fanyakazi zao, karibia miaka miwili imepita tumejaribu kutathimini je kuna maendele yoyote yamefanyaka katika hili swala? stylist wanafanya kazi zao vyema kabisa lakini upande wa wabunifu bado tunachechemea, well leo tumeamua ku throw back na hili andiko labda safari hii wataelewa na kulifanyia kazi

Ime fika muda wa Africa ndani yake tukiwemo wa Tanzania tujue kuna tofauti kubwa mno kati ya mbunifu, stylist na fundi cherehani japo wote wana deal na kitu kimoja mitindo.

Si kila mbunifu ana weza kuwa stylist, si kila fundi cherehani ni mbunifu na si kila stylist ni mbunifu.

tujue kwanza tofauti za watu hawa

Mbunifu huyu ni yule anae chora michoro ya mavazi ana buni vazi liweje kwa kuliweka katika karatasi, huyu ana jua kitambaa gani kitumike, kipi kikae wapi na kipi kikaeje

Fundi cherehani huyu ni baada ya mbunifu kubuni yeye ana pelekewa kushona ile nguo, ana kata makato ya kitambaa na kushona ili ile idea ije iwe reality katika dunia

Stylist huyu yeye baada ya mbunifu na fundi cherehani kufanya kazi zao yeye ana mstyle mtu kwamba nguo hii itanedana ukivalia na kiatu hiki, shati rangi hii na urembo huu. Hawa ni watu watatu tofauti ambao kwa pamoja wana fanya ulimwengu wa mitindo uendelee kuendelea

kilicho tufanya mpaka tuka andika hili ni jinsi ambavyo wasanii wetu wana shindwa kuelewa, week chache zilizo pita kuna baadhi ya wasanii wali tangaza kuwa wana valishwa na baadhi ya watu tulikua na expectations kubwa sana kutoka kwao lakini kuna walio tufurahisha na walio tufanya tuandike hii article leo

Shilole alitangaza kuvalishwa na Kikifashion na Martin Kadinda hawa wote ni wabunifu wakubwa sana Tanzania na tulitegemea callable yao itatoa kitu bora sana lakini imekua tofauti

 

Shilole/Shishi ame buniwa nguo hatuwezi kusema ni mbaya labda kama kunge kuwa na mkono wa stylist ingekaa vizuri au kuvaliwa vizuri zaidi ya hivi alivyo vaa

4 14052464_1470538442973380_1382229477_n

Weusi, weusi walitangaza kuvalishwa na cutrite designs ukitembelea instagram yao huto ona sehemu wame andika kama wao ni ma designer, stylist au mafundi cherehani ila kwa kuangalia utajua hawa ni washonaji, wame washonea nguo weusi lakini hawaja wa style wala hawaku buni vizuri

hii ni show ya Fiesta ya nyuma una weza kuona weusi walivaa walikua coordinated as a group, simple ila wame pendeza

IMG_8424

hii ni mwaka huu ambapo wame valishwa na mtu binafsi unaweza kuona kuna tofauti kubwa sana hamna uwiano, kila mtu kavaa kivyake rangi haziendani yani its a mess

14027141_1633066290336944_2094298550_n

on the other hand Maua… Maua ame valishwa na the stylist studio.. hawa ni ma stylist pia kuna mbunifu ndani yake ambae ni Rio, Tuna weza kusema Maua me improve alot kutoka alipo kuwa zamani mpaka sasa hata kama nguo zake kime nunuliwa dukani hazija buniwa na the stylist lakini wame mtendea haki Maua, kila kitu kipo on trend na she looked stylish.

Maua kabla ya the stylist

12907190_1665361390394530_183672919_n

Maua baada ya the stylist

14063522_285434175165390_1125043646_n 14099334_1159156480772676_1554180132_n

Tuna dhani mme elewa nini tunaongelea kama una maoni una weza kutuachia hapo chini, na pia una weza kutupata katika mitandao ya kijamii

Facebook- afroSwagga

Twitter -Afroswaggatz

Instagram- Afroswagga

Related posts

2 Comments

  1. สล็อต

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/tofauti-ya-mbunifustylist-na-fundi-cherehani/ […]

  2. what type of mushroom is penis envy

    … [Trackback]

    […] Here you will find 16827 additional Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/tofauti-ya-mbunifustylist-na-fundi-cherehani/ […]

Leave a Reply