Kwa kiswahili vyote huitwa mitindo lakini kwa kingereza huitwa Style na Fashion hizi zina tofauti kubwa mno ambayo wengi hatujui kutofautisha. Utasikia mtu akisema nime penda style yake au nime penda fashion yake bila kujua tofauti ya maneno hayo mawili.
Style: hiki ni kitu ambacho umezaliwa nacho, unacho moyoni mwako hakinunuliki dukani wala hakibadiliki. Style ni namna mtu ulivozoea kujiweka, vile unavopenda uwe na utafsiriwe. Style kiujumla ni utambulisho wako haswa kwenye muonekano.
Kwa mfano Salama Jabir style yake ambayo tume mzoea nayo ni nguo za kiume mara nyingi hupendelea kuvaa hivyo ni mara chache kumkuta amevaa nguo za kike hii ni style ya salama kitu ambacho ame zaliwa nacho hawezi kukibadilisha wala haja kinunua dukani
Fashion: ni mitindo ambayo hubadilika na ina nunuliwa tunaweza kumtolea mfano huyu huyu salama, salama style yake ni nguo za kiume lakini hizo nguo za kiume zina fashion yake leo atavaa suruali ime chanwa magotini kesho ime pindwa chini ya miguu nk. lakini havai zile za kike bali huvaa za kiume.Pia Fashion huja na hupita lakini style haipiti, ni vema ukawa una style yako ya kuvaa inayokupendeza kiasi kwamba ikija fashion fulani basi unaangalia kama inaendana na style yako.
Related posts
2 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/tofauti-ya-style-na-fashion/ […]
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/tofauti-ya-style-na-fashion/ […]