Imekuwa kawaida sasa kwa wabunifu kuwa wana copy-iana kazi zao, sikuhizi hatuiti copying bali tunasema kuwa inspired, hivi karibuni brand ya  Versace imewashtaki brand ya Fashionnova kwa ku-copy hili gauni ambalo ni Iconic dress kutoka katika brand yao.

Fashionnova Yashtakiwa Na Versace Kwa Kucopy J Lo’s Iconic Jungle Print Dress

Gauni hili lilivaliwa na mwanadada Jennifer Lopez mwaka 2000 katika red carpet ya Tuzo za Grammy na ilifanikiwa kuongelewa sana kiasi ambacho mwaka jana walii-upgrade na kumtumia Jlo kuivaa katika show yao.

Well hatujui kama mwanadada kutoka Nigeria, Toke Makinwa na mbunifu Tolu Bally ( 2207bytbally ) waliisikia hii habari au wameisikia na kuamua kuipuuzia.

Jana mwanadada Toke alipost hii picha katika mtandao wake wa Instagram akiwa amevalia gauni linaloendana kama lile la J lo kutoka kwa brand ya Versace akiwa anaenda kuhudhuria katika #Anightwiththestars2019 event

Well hii ikatufanya tufikirie will Versace sue them too? na ni lini tutaacha hii tabia ya ku-copy kutoka kwa wengine? tena basi tuna-copy kila kitu mpaka fabric? ni vipi unajiita mbunifu kama unachukua ubunifu wa wengine?

Well Afromates tupe maoni yako katika hili unadhani ni sawa mbunifu ku-copy kazi ya mwenzie?