Ule muda ambao wengi wenu Afro mates mnaupenda ndio huu, muda ku-review nini tumekiona kutoka katika Swahili Fashion Week, mbunifu yupi alipandisha kipi na kama tumekipenda au lah, vitu gani na gani tumeona vya tofauti na kuvipenda na vipi vili-trend, tupo hapa kwa ajili yenu na hapa tunawaletea trend ambazo tumeziona na pieces ambazo tumeona ni unique.
Tuanza na trend zipo tano ambazo tumeona zimejirudia kwa wabunifu zaidi ya wawili
Rangi ya njano ilikuwa all over, iwe mustard yellow, lemon yellow, wabunifu wengi wameonekana kutumia rangi hii na ilipendezesha jukwaa kutoka kwa wabunifu mbalimbali, njano ni moja ya rangi ambayo ni nadra kuona watu wamevaa labda kwa sababu ya uniqueness yake ndio maana wabunifu wameamua kuitumia kuonyesha namna gani unaweza kuitumia, lakini pia ni rangi ambayo ili trend sana kwa wenzetu mwaka huu.
Mahdish Fashion Designer akiwa ametumia rangi hii
Kiki Fashion na yeye alitumia hii rangi katika collection yake
Mbunifu Lucky creations na yeye alitumia hii rangi.
brim hats ni zile kofia hutumiwa hasa kwa waendaji wa beach, horse riders etc lakini talking about fashion, every thing is possible kwa sasa unaweza fika nazo hata katika red carpet au kuvaa on a dinner date as they say fashion is what you buy style is what you do with it. tumeona wabunifu wetu wakitumia sana kofia hizi katika collection zao kuna wale ambao walienda extra miles kwa kutengeneza kubwa, walio jaribu ku-spice up na prints mbalimbali na wale walioamua kuwa traditional
capellas_fashion.tz yeye aliamua kutengeneza hizi very wide brim hats to hide from your haters
afrisolo fashion gave us a kitenge brim hat
wakati mbunifu kisusi yeye alichagua kutumia straw traditional brim hats.
Trend nyingine ambayo tumeona ni wabunifu kutengeneza mavazi yenye majina yao, yaani kama vile ambavyo unavaa shirts au t-shirts zenye majina ya wabunifu wakubwa duniani kama Gucci, Channel basi ndivyo na huku kwetu wameamua kufuata utaratibu huo, trend hii tumeona kwa wabunifu mbalimbali akiwepo
Afro retro kama ambavyo unaona yeye ametumia kwenye hii long sleeve tee, mbele utaona ametumia maandishi ya kampuni yake.
Samuel Zebedayo yeye ali-debut mavazi ya aina nyingi yenye logo la jina lake zikiwepo boxers, skin tights, belts na vingine vingi.
Neste Fashion nao walitupa hii style kwa namna yao.
Enji Maasai with the kitenge Logo
Traditional bags an outfit isn’t complete without a perfect statement bag, tulichokiona kime trend katika swahili fashion week 2018 ni traditional bag iwe safari bags za vitenge, clutch za vitenge au animal printed bags lakini pia tumeona vikapu vikipitishwa kwenye run way as we all know kikapu kimekuwa kikitumiwa sana sasa hivi na ma-fashionista kama handbag
Bijoux trend
Kisusi Designs
The mabinti centre
Half short, half long sleeves fashion, tumeona style kwa wabunifu mbalimbali ambapo nguo moja inakuwa na style mbili ikiwa mkono mmoja umekatwa na mwingine ukiwa na mkono mzima, ni kama nguo za aina mbili zimeunganishwa pamoja, very creative na inaweza kuja kuwa trend kubwa mwakani.
shabaaz sayed
Tuambie ni trend gani imekuvutia katika hizi?
Related posts
HOT TOPICS
Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/VZ1jH2zJUg
FollowHappiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/689j7Yjcn0
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
Feza Kessy Atuelezea Kuhusu Fashion & Style Zake
Feza Tadei Kessy ni Muimbaji, Muigizaji lakini pia ni mtunzi wa nyimbo lakini pia Fezza ni former beauty queen ambapo mwaka 2005 alikuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala & Miss Tanzania Runner up. Lakini pia alishawahi kuwepo katika Reality Tv Show – Big Brother Africa. Kwa…