SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Tuchukue Jibu Gani Kutokana Na Ukimya Wa Basata?
Mitindo

Tuchukue Jibu Gani Kutokana Na Ukimya Wa Basata? 

Hivi karibuni Miss Tanzania organization walimvua uwakilishi wa Miss World, Miss Tanzania 2020/2021 Rosey Manfere ambae alifikisha swala hili katika Baraza la Sanaa Tanzania. Baraza walitoa Tamko ya kwamba Rosey anafaa kuwakilisha Nchi katika mashindano hayo.

Lakini Miss Tanzania Organization walipinga swala hili na kusema kama Basata wataendelea kumtetea Rosey basi watafikishana mahakamani.

Well kilichotuulizisha leo hapa tuchukue jibu gani kutokana na ukimya wa Basata katika swala hili kubwa ni kwamba kwenye Barua ya Basata kwenda kwa Miss Tanzania Organization iliandikwa kutakuwa na kikao cha pande zote mbili Tarehe 23.7.2021.

Leo ni tarehe 27.7.2021 siku takribani nne zimepita toka tarehe husika ambayo ilitakiwa kufanyika kikao hiko. Kwakuwa swala hili linahusu wa-Tanzania kwa ujumla imebidi tuulize kwa niaba Je, Ukimya wa Basata unatupa jibu gani? Wamekubaliana na Rosey kutokuwakilisha Nchi au bado wana Msimamo wa Rosey kuwa muwakilishi? As they say Ukimya nalo ni jibu lakini je ni jibu gani?

Related posts