Lagos Fashion Week Na South Africa Fashion Week zimefanyika week iliyopita na ukweli usemwe wenzetu wanajitahidi sana katika kutumia hii nafasi vizuri kujitangaza, na hii sio tu wabunifu bali wanamitindo, fashionista’s, fashion bloggers na wadau wa mitindo kiujumla.
Sisi tulikuwa tunaangalia nini ambacho wanafanya na kitu gani tunaweza kujifunza kutoka kwa wenzetu, tulichogundua ni kwamba ni vitu vilevile ambavyo sisi huwatunashauri vifanyike katika Swahili Fashion Week ndivyo vinavyotumiwa na wenzetu ili kufanya tamasha hili kuwa na hamasa na watu kuwa attention nalo.
- Wabunifu Kuwa Creative
Tunadhani wabunifu wetu wajaribu kuangalia namna ambavyo wana show case collection zao, designs tofauti, material tofauti huwezi kukuta collection ya fulani ina fanana na fulani, wanatofautiana, lakini pia wapo creative katika designs zao sio zilezile ambazo tumezoea kuziona kila siku wanajaribu kuweka utofauti wa kile ambacho tumezoea ana kishona na kile ambacho ana show case katika runway
safw designer @palesamokubung
- Utumiaji Wa Stylist
Kama ukiangalia collection za wenzetu utaona kabisa kuna stylist behind the collection, namna ambavyo models wana kuwa styled ni tofauti kabisa na sisi, kwa sababu imeshonwa two pieces basi ndio inavaliwa hivyohivyo wenzetu wanajitahidi katika kuongezea accessories kuongezea naksi ili kuleta utofauti.
LFW designer @nack_apparel
- Mabadiliko Ya Models
Kwetu model akipanda na style ya nywele, viatu na makeup basi kila collection ya siku hio atapanda navyo hivyohivyo hakuna mabadiliko ambayo utayaona, kama mbunifu unahitaji kujua vazi langu fulani nataka model avalie kiatu fulani ili kuendana na collection yako, lakini utakuta kila collection model ana kiatu kilekile wakati mwingine kiatu hata akiendani na vazi, ili mradi tu anaviatu miguuni,tofauti kabisa na wenzetu wao wanakuwa wamejiandaa vilivyo
- Kutumia Watu Maarufu Katika Run Way
Both Lagos & South Africa Fashion Week wametumia watu maarufu katika runway zao, hapa sio kwamba waandaaji ndio waliwaandaa hawa watu maarufu hapa, wabunifu waliwaongea na hawa watu maarufu na kupanda katika ku-show case collection zao, Nigeria tuliwaona BBA Nigeria Bam Bam Na Tobi Bakre wakiwa wamepanda kwenye runway
wakati South Africa tuliwaona Fashion Influencers Enhle Mbali Maphumulo,Sarah Langa Mackay pamoja na Kefilwe Mabote kuwaona watu maarufu katika runway kuna wahamasisha watu kuja kuona kesho kutakuwa na nini lakini pia watu kuongelea kwamba fulani alipanda katika jukwaa na fashion week fulani na alifanya nini, inaleta aweraness katika society.
- Muamko Wa Watu Maarufu Katika Hizi Event Ni Mkubwa
Tuliliongelea hili kwamba Swahili Fashion Week watu maarufu wana attend siku ya mwisho tu ya Tuzo, mwaka jana tuliona mabadiliko kutokana na ugawaji wa Tuzo ulikuwa tofauti lakini kwa wenzetu tumeona miamko kutoka kwa watu maarufu kuhudhuria katika event hii, na wana slay haswa ukiangalia jinsi ambavyo wamevaa mavazi yao lazima uamini kwamba wanamuamko na hiki kitu, tofauti na kwetu watu maarufu hawana muda na hii event, kuanzia bloggers, stylist, fashionista ni wachache ambao wanahudhuria na mpaka awe anawania tuzo au kaalikwa na hata wakihudhuria wanakuwa tu kawaida hawaonyeshi kama wapo katika hii event, wenzetu ni tofauti watu maarufu wakubwa wame attend kuanzia Rita Dominic muigizaji mkubwa Nigeria, stylist& Fashion Consultant Dénola Grey,
Muigizaji Ini Dima-Okojie
lakini pia South Africa Fashion Week napo vivyo hivyo.
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/tujifunze-kutoka-lagos-fashion-week-na-south-africa-fashion-week/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/tujifunze-kutoka-lagos-fashion-week-na-south-africa-fashion-week/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/tujifunze-kutoka-lagos-fashion-week-na-south-africa-fashion-week/ […]