SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Tunahitaji Fashion Influencers Kukuza Fashion Industry Ya Tanzania
Mitindo

Tunahitaji Fashion Influencers Kukuza Fashion Industry Ya Tanzania 

Moja kati ya vitu ambavyo vina angusha industry ya fashion Tanzania ni kukosa fashion influencers na hapa hatumaanishi celebrities au stylist, hawa ni wale watu wa kawaida tu ambao wanapenda mitindo, hawa huwa wakati wengine tunawaita fashionista’s ni wale watu ambao wanaweza kuvaa vazi la kawaida na kulipendezesha au kunogesha zaidi.

Hawa kazi yao ni ku-inspire wengine katika mavazi na wao huwa wanatumia high & low end ili kubalance wale wanao vaa mavazi ya kawaida na wale ambao wanauwezo wa kuvaa brand za dharma. Nchini kwetu hawa watu wapo wachache mno, ukiangalia kwa wenzetu unaweza kukuta wapo influencers zaidi ya thelasini ambao kazi yao ni kuvaa tu na kuonyesha how to do it.

Tunadhani hii ni moja kati ya vitu ambavyo vinafanya Tanzania tusionekane fashionable maana tuna depend na celebrities ambao ni wachache mno wanaojua kuvaa vizuri, in order for a country to be counted as fashionable huanzia kwa wananchi wa chini lakini ni vipi ambavyo unajua wananchi wake wanavaa wakapendeza? ni pamoja na kuwa na influencers ambao wao watawawakilisha wananchi wote.

Influencers ambao tunao ni wachache lakini pia they are not that deep kwenye kutoa tips kwa wengine, wengi wanavaa wao waonekane wamependeza. Wakati nchi za wenzetu wengi wanajitaidi kuwa wanatoa tips kwa wengine on how you can dress up katika hafla mbalimbali, lakini pia unaweza kuongezea kipi kwenye mionekano wako, namna tofauti za kuvaa outfit moja, hii husaidia wale wengine ambao hawajui wafanye nini kupata mwangaza.

Ukiangalia kama South Africa, Nigeria, Ghana wana fashion influencers wakutosha na sisi tunaiga kutoka kwao, a fashion influencer haitaji kuwa na pesa nyingi anacho hitaji ni uwezo wa kujua how to dress up hii inaweza kuwa hata wewe ambae unasoma hapa.

Fashion Influencer ni daraja kati ya brands na jamii, lakini pia ni daraja kati ya fashion na jamii wao husaidia jamii kujua ni brand gani ina bidhaa nzuri japo huwa wanalipwa kuzisifia, lakini pia husaidia jamii kujua ni vipi wavae na nini kina trend, Tanzania tunauaba wa fashion influencers.

Related posts