SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Tunatengeneza Aina Gani Ya Kizazi Cha Wabunifu Wa Baadae?
Mitindo

Tunatengeneza Aina Gani Ya Kizazi Cha Wabunifu Wa Baadae? 

Fashion Industry ya Tanzania bado ina mengi ambayo yanaenda ndivyo sivyo, na tukiongelea fashion indusrty tunamaanisha industry nzima kuanzia models, stylist, designers, photographers na wengine wote wanaoingia katika category hii, leo tunaongelea kuhusu wabunifu hawa wa kwetu wa sasa kutoka Tanzania Je wanatengeneza kizazi gani cha wabunifu wa baadae?

Kwa sasa hivi ukiuliza mbunifu ndoto yako ni kuwa kama nani baadae, asilimia 70 watawataja wabunifu wa zamani, utasikia Mustafa Hassanali, Ally Rehmtulla,Martin Kadinda, Khadija Mwanamboka na wengine wengi, lakini swali linakuja Je kwa wabunifu ambao wanachipukia watataja hiki kizazi cha sasa cha wabunifu kama role models wao?

Inaweza ikawa zamani hakukuwa na technologia ya wengi kugundua fulani ameigia mshono au ubunifu na ndio maana wengi tulikuwa tunawaona wao kama hero’s wetu linapokuja swala la ubunifu lakini kwa sasa kila mtu ana smart phone kila mtu anajua huu mshono nilisha uona sehemu haiwezekani ikawa ni original design, lakini pia wabunifu wenyewe wanaoiga design za watu hawaoni aibu kutamka peupe mbele za watu kwamba wamecopy na wapo proud of it.

like seriously unajiita mbunifu lakini upo okay ku-copy kazi ya mtu na kutamka hadharani kwamba umefanya, haya wale ambao wanakuja wakiona kwamba wewe tu mkubwa umecopy na your okay with it basi yeye ni nani hata asumbue kichwa kwenye creativity? hapo ndipo wenzetu Nigeria na Nchi nyingine wanapo tuacha nyuma.

Lakini pia wabunifu kubagua watu wa kufanya nao kazi na kuchelewesha kazi za watu, hili ni jambo ambalo linalalamikiwa sana, kwa kuwa wanavalisha watu maarufu basi wengine wanadharaulika,

let’s say hao watu maarufu unawavalisha ili upate nini? kujulikana halafu ukisha julikana? upate wateja right? sasa kwanini wanapokuja wadharauliwe? Jiulize kwanza kwanini mteja kakuchagua wewe hata kama kaona mishono ya watu zaidi ya hamsini huko nyuma? kwamba amependa kazi na angependa kukusupport kitu kikubwa ambacho leo Mustafa kawa Mustafa, au Ally Rehmutulla, Sheria Ngowi na wengineo ni heshima katika kazi zao, wana nyenyekea wateja wabunifu wa sasa wamekosa heshima na kazi zao hii inatufanya tufikiri wajao watakuaje?

Inawezekana ikawa sawa kwenu kwa sababu kwa sasa nyinyi mpo kwenye indusrty mna hit lakini tuseme tu ukweli haya mambo yanabomoa industry kila siku inazidi kumomonyoka, wenzetu ambao walifanya effort hivi vitu visionekane kuwa uhuni wanaaibika sasa, wameanza na kujenga foundation nzuri kwa sababu ya kizazi kijacho lakini kizazi hiki walicho kijengea ndio wanawathibitishia wale ambao wanasema hii industry ni uhuni walikuwa hawajakosea, lakini pia haina haja ya kujiita mbunifu kama hujui ethic zake jiite tu mshonaji we will understand, kuna tofauti kubwa ya mbunifu na fundi juma mtaani ukiachana na kubuni mbunifu hawezi acha mteja wake asipate vazi lake kwa wakati, ni muda wa kuamka na kujifunza.

 

 

 

 

Related posts

3 Comments

  1. พนันบอล

    … [Trackback]

    […] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/tunatengeneza-aina-gani-ya-kizazi-cha-wabunifu-wa-baadae/ […]

  2. Blue Meanies – 4 Oz

    … [Trackback]

    […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/tunatengeneza-aina-gani-ya-kizazi-cha-wabunifu-wa-baadae/ […]

  3. weed delivery toronto

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/tunatengeneza-aina-gani-ya-kizazi-cha-wabunifu-wa-baadae/ […]

Comments are closed.