SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Uhusiano Kati Ya Muziki,Filamu Na Mitindo
Mitindo

Uhusiano Kati Ya Muziki,Filamu Na Mitindo 

Imekuwa muda sasa tumekuwa tunasisitiza kuhusu mionekano ya watu maarufu katika Tasnia za muziki na filamu, wengi wamekuwa wakiuliza kwanini? well leo tumeona tuwaletee kwanini huwa tunaangalia sana mionekano ya watu maarufu katika sekta hizi mbili, ni ukweli usio fichika kuna uhusiano mkubwa sanakati ya hizi tasnia mbili na mitindo.

 

  • Style/Fashion Hutumika Kutofautisha Wanamuziki/Waigizaji

Miaka ya 2000 mwanzoni hapa ndipo Bongo flava na movie Nchini vilikuwa vinanoga na kuanza kuja kwa kasi, wanamuziki wengi tulikuwa tunawatofautisha kutokana na style zao za sauti lakini pia mavazi, kipindi hiki tulikuwa tunamjua T.I.D ambae yeye styles zake always ziko fresh japo sio trending styles, T.I.D ni moja kati ya wasanii ambao hupenda kuonekana classy. Lakini pia Mwana Fa na Ay hawa walikuwa na zile hip hop styles ambapo mtaani vijana wengi walikuwa wanapenda kuvaa, long oversized t-shirts, over size trouser au pants na sneakers, well hii pia ilikuwa inaoneka Marekani  kwa wasanii kama kina 50 cent, The Game na Solder Boy wengine wengi.

Miaka ya 2010 kuja juu tukawapata watu kama Diamond Platnumz ambae yeye alikuja na colorful style, nani hakuvaa colorful skin jeans na long tee? sio kwa upande wa wasanii wa kikeni na kiumeni wote walivutiwa na hizi styles na kuvaa, Lakini pia upande wa movies Ray Kigosi na Marehemu Steven Kanumba (R.I.P) nao walikuwa na vibes zao za suits za ming’ao (kicongo man ),tunacho jaribu kusema ni kwamba japo Mitindo inaanzia kwa fashion genius ambao ni wabunifu lakini pia wasanii wa muziki na movie wana contribution kubwa ya kufikisha hii sanaa kutoka kwa wabunifu kuifikia jamii, lakini pia jinsi ambavyo unaonekana ndivyo ambavyo tunaona value yako na utofauti wako.

  • Fashion Labels Hutumia Wanamuziki/Waigizaji Katika Kutangaza Kazi Zao

Iwe katika wimbo au movie yako uvae bidhaa yao au hata katika mavazi yako ya kila siku, fashion labels huwa wanatumia waimbaji na waigizaji kutangaza bidhaa zao hii kutokana na kwamba ni rahisi kufikia walengwa, kwa sababu wasanii ni kioo cha jamii. Tukiangalia kama sasa hivi ambapo fashion labels nyingi zinajaribu kufika Africa wanatumia wasanii kutoka Africa kutangaza kazi zao,Wiz Kid Ayo kutoka Nigeria ni mfano mzuri tumemuona mwaka huu akitumika na fashio brand kama Nike ambao wamefanya nae katika kombe la Dunia lakini pia kutembea katika runway ya Dolce & Gabanna na sasa kuonekana katika Circoc X Moschino Collaboration,

tunajua ni kwamba Wizkid is making all this waves kwa msingi alio jiwekea chini kama asingekuwa anaonekana fashionable katika mionekano na kutafuta collaboration na wanamuziki wa nje basi hizi deals nazo asingezipata this is why tuna wekea mkazo katika mionekano ya wasanii wetu.

 

  • Trend Setting

Huwa tu hatuangalii movie au music videos sababu ni sehemu ya burudani lakini pia kujifunza nini kimevaliwa katika videos hizo, mfano nani angejua kama unapoenda katika event zenye mziki wa taratibu kuna mavazi yanatakiwa uvae, kama unaenda kwenye hip hop kuna aina yake ya mavazi, segere, ngoma etc kama isingekuwa kwa kuona katika music videos zenyewe au movies? yah right ni huko kupitia kina Michael Jackson, kupitia kina LL Cool J, Missie Eliot, Celine Dion na wakongwe wengine wengi tukajua kumbe hapa unatakiwa kuvaa hivi na hapa ni hivi japo fashion haina mipaka lakini how can you dance a move bish song in a long tail dress?

Well tunaweza kuendelea na kuendelea kuandika kuhusu hii topic lakini haya ni mambo matatu makuu ya kuna uhusiano gani kati ya fashion na muziki na movie’s, kama ni watu wa kujifunza tunaweza kujifunza kutoka kwa watu maarufu kama Rihanna hajatoa muziki mpya lakini we all see her slaying & talk about it, wakati wengine wakienda kwenye OTRII ya Beyonce na Jay Z kusikiliza muziki wegine huwa tunaangalia watakuwa wamevaa nini, wakati wengine wakimmiss Elizabeth Michael kwenye uigizaji wengine wanamiss kuona mitindo yake ya mavazi.

Related posts

3 Comments

  1. wegovy results before and after​

    … [Trackback]

    […] Here you can find 33492 more Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/uhusiano-kati-ya-muzikifilamu-na-mitindo/ […]

  2. 티비위키

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/uhusiano-kati-ya-muzikifilamu-na-mitindo/ […]

  3. คาสิโนออนไลน์

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/uhusiano-kati-ya-muzikifilamu-na-mitindo/ […]

Comments are closed.