Yapata karne moja (kwa muda wa miaka 98 hazija wahi kubadilishwa),Kampuni ya Nike imeamua kufanyia marekebisho viatu vyake aina ya Converse’s Chuck Taylor All Stars kubuniwa tena kwa mtindo mwingine wa kisasa zaidi. Wengi wanasema ni kufuru kufanya marekibisho katika viatu hivi kwa maana bado mtindo wake haujapotea na unapendwa kila kukicha watu wa rika tofauti tofauti. Lakini mtindo huu mpya hauto utoa sadaka mtindo wa zamani ulio zoeleka.
Viatu aina ya Converse Chuck II vitakua madukani kuanzia wiki ijayo, Viatu hivi vitapatikana katika rangi nne nyeupe, nyekundu, buluu na nyeusi pia vitauzwa kwa $70 (140,000 tzs) kima cha chini na $ 75(150,000 tzs) kima cha juu. Teknologia itakayo tumika ni kutoka katika kampuni yake mama, aina hii mpya ya vitakua vya chini (sio virefu), vyenye rangi za kuvutia zaidi na kuongezea msaada wa uzito katika viatu hivyo.
Marekebisho makubwa katika hivi viatu aina ya CTASII (Converse’s Chuck Taylor All Stars) ni kuongezewa sock liner ambayo imetengenezwa kwa lunarlon na nyenzo nyingine ambazo zimeshawahi kutumika katika aina nyingine za viatu vya Nike ambavyo vilikua maalumu kwa ajili ya wanariadha. Mkurugenzi mtendaji wa converse bwana Jim Calhoun alisema kuwa “humu duniani watoto wanakua wakiijua faraja- kutegemea faraja- na hawapendelei usumbufu”.

Related posts
HOT TOPICS
We need to have some sort of bima ila for enjoyment. Yaani wanakata ka % ka mshahara kako unakua na card ukienda se… https://t.co/W9oDoaN2YY
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…