Hivi ni vigezo gani vimetumika kwa Lemutuz kuwa official Judge wa Miss Morogoro 2018? Tuseme tu sio morogoro bali mkoa wowote ule, Lemutuz anawezaje kuwa judge na kuchagua Miss anaefaa? Kuna vitu vinachekesha kuchekesha katika uhalisi wa mambo jinsi sasa ambavyo Miss Tanzania inaendelea kufanyia katika ngazi ya Mikoa.
Moja ya shangazo kuu ni Lemutuz kuwa official Judge wa Miss Morogoro, hivi wametumia vigezo gani kumpa?. Au wametazama kwa kuwa huwa anapost wabebez basi wakaona anafaa kabisa kuwa Judge katika mashindano hayo? (Aibu).Kwanini wasitumie watu wenye ujuzi na mambo hayo? kwa maana ya mamiss ambao walishapita katika uwanja huo? Mfano Morogoro yupo Flora Florence ambaye aliwahi shinda kitaifa Multichoice Miss Talent 2010, kwanini wasimtumie mtu kama huyo kiasi wamtumie Lemutuz?
Kama kweli tunataka tuendelee ni vyema kutumia watu wenye ujuzi, ubabaishaji katika swala zima la urembo halitaweza kutusaidia bali kuzidi kuua tasnia kwa ujumla. Tunalia kila siku serikali iangalie na uwanja wa urembo pia wakati sisi wenyewe ndio tuna yashusha hadhi haya mashindano, Inakuwaje umuweke mtu ambae hata hajui kinacho endelea na kuwaacha wajuao? Je unadhani utapata chaguo sahihi la watu kufurahia mpaka serikali ikaamua kusaidia? Tulitegemea kuona former miss, au watu wanaohusiana kiundani katika mitindo, Hakika mkistaajabu ya Rukwa mtayaona ya Morogoro ya Lemutuz kuwa Official Judge.
Sisi tunaendelea kutafakari ni vigezo gani vimetuka kwa Lemutuz kuwa Official Judge wa Miss Morogoro 2018, kiasi cha kuachwa kwa watu wenye ujuzi katika mji huo?
Related posts
4 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/ukistaajabu-ya-miss-rukwa-utayaona-ya-lemutuz-kuwa-official-judge-miss-morogoro/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/ukistaajabu-ya-miss-rukwa-utayaona-ya-lemutuz-kuwa-official-judge-miss-morogoro/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/ukistaajabu-ya-miss-rukwa-utayaona-ya-lemutuz-kuwa-official-judge-miss-morogoro/ […]
… [Trackback]
[…] Here you can find 69232 more Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/ukistaajabu-ya-miss-rukwa-utayaona-ya-lemutuz-kuwa-official-judge-miss-morogoro/ […]