SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Umuhimu Fitting Katika Mavazi
Mitindo

Umuhimu Fitting Katika Mavazi 

Mavazi yaliyoshonwa vizuri yanaweka utofauti mkubwa katika muonekano wako, lakini mavazi yanayokutosha vyema, hapa tunamaanisha mavazi ambayo yanakupa nafasi ya kupumua bila kubana sana wala kuachia sana, mavazi yanayoishia urefu sehemu sahihi yanakufanya uonekane zaidi ya yale yaliyoshonwa vyema.

Fitting Ya Mavazi Imegawanyika Katika Sehemu 3

  • Loose Fitting / Mavazi Mapana

Haya ni yale mavazi yanayokuachia kwa kiasi kikubwa, unakuta suruali au shirt pana au refu kuliko mwili wako.

  • Tight Fitting / Mavazi Yanayobana

Haya ni yale mavazi ambayo ni madogo kupita mwili wako, yaani unakuta umebanwa kiasi ambacho huwezi kupumua au kufunga vifungo/zip vyema

  • Great Fitting / Mavazi Yanayokutosha Vyema

Haya ni yale mavazi ambayo yanakutosha vyema, yanakupa upana sahihi wa kupumua bila kuzidi udogo au ukubwa, mavazi ambayo yanendana vyema na mwili wako.

Unaweza kujiuliza haya mavazi yanayoendana na mimi nitayatoa wapi? Wakati watu maarufu wengi hasa wa Nje wanakuwa na mavazi ambayo ni custom made kwahio si rahisi kukuta wanavaa ill fitting lakini pia kuna mafundi cherehani ambao wanaweza kukusaidia kufanya vazi lako likakutosha vyema endapo ni kubwa likapunguzwa au kama ni dogo na linanafasi ya kuongezwa.

  • Kwanini Mavazi Yanayo Kutosha Vyema Ni Muhimu?

Mavazi yanayokutosha vyema ni muhimu kwasababu mara tu unapokutana na mtu anaku-judge kutokana na muonekano wako, ukionekana na mavazi makubwa au madogo kuliko wewe basi itampa mtu huyo mawazo ya kwamba hujielewi, how come mtu anajielewa anatoka nyumbani kavaa nguo kubwa au ndogo kuliko yeye mwenyewe?

Mavazi ambayo unavaa yakuelezea wewe ni nani, endapo utavaa mavazi makubwa kuliko wewe inaweza kuelezea kwamba hujiamini na unajaribu kujificha ndani ya mavazi yako lakini pia ukivaa yale madogo kuliko wewe inaweza kutupa picha umepotea hujui nini ambacho unafanya.

Ukiangalia watu maarufu wengi wanatumia hii njia katika mavazi yao, wengi hawakunji kunji mavazi kama jeans kukunja chini au kukunja mikono kwasababu mirefu sana, unaweza kukuta mtu maarufu amevaa tu T-shirt na jeans lakini amependeza mno, japo kuna extra kama accessories lakini fitting nayo huchangia.

Kuvaa mavazi ambayo yanakutosha haikufanyi tu ujiamini bali pia ni namna nzuri ya kuonyesha umbo lako hasa kama utavaa mavazi yanayokutosha vyema na yanaendana na umbo lako.

Related posts