SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Umuhimu Wa Nguo Za Ndani Sahihi Katika Muonekano Wako
AfroTipAndTricks

Umuhimu Wa Nguo Za Ndani Sahihi Katika Muonekano Wako 

Lets talk about dressing na namna nguo hukaa kwenye mwili. Wote tunapenda kuonekaana kama kasnack fulani ndani ya nguo, ndio maana tunavaa vizuri hata hivyo wengi wetu tunapenda assets zetu zikae sawa ndani ya nguo. Unaona all those celebrities wanavyovutia wakipita kwenye red carpet? Wether nguo iwe na mkono mmoja, mikanda, mgongo wazi n.k bado mwili unaonekana flawless? Kama uko makini sana utakuwa umenotice kuwa nguo hukaa mahali pake hata kama mtu ni mnene sana. That’s the power of the right undergarment. Hii haiko kwenye red carpet tu na nakuhakikishia kuwa hii si muhimu kwa plus size women tu. Binadamu ni binadamu tu, you can be super hot lakini kuna nyama huwa hazitaki tu kukaa mahali pake. We have celebs kama Kim Kardashian na Beyonce, wako so sexy lakini ni moja ya watu ambao wanatumia undergarment.

Nguo yako inavyokaa katika mwili wako has a lot to do na mavazi uliyovaa ndani ya nguo hiyo. Unfortunately baadhi ya undergarment zimekuwa hazichukuliwi serious sana na nyingine ni taboo bongo. Let me tell you something, hata faves wako wanavaa undergarments. Ukiangalia nigerians, utanotice wengi wanapendeza sana katika mavazi. Tofauti na sisi, Nigerians hupenda sana undergarments so kukuta mtu kavaa belt ya tumbo ni kawaida. Why should you suffer, uache kuvaa nguo unayoipenda kwasababu ya tumbo, au nyama ya kiunoni? Nataka kukuonesha nguvu ya mavazi ya ndani because babe! They are powerful. Here we go;

 • Zina Boost Confidence

Hakna kitu humfanya mwanamke ajiamini kama the right outfit ikiambatana na the right undergarment. That feeling you get umapojua the twins wamekamatiliwa vizuri kifuani. Mikanda ya braa iko mahali pake. Hakuna four boobs kifuani. Mikanda haionekani wala kuharibu look ya nguo.

Ile amani unayopata unapojua tumbo limebana halining’inii, mwili hauchezi na kurukaruka ovyo, mashimoshimo kwenye mwili hayaonekane. Ile kujua tu kila kitu kuhusu outfit yako kiko sawa huongeza kujiamini. Kuna namna nyingi sana undergarments husaidia katika hili. The right bra hufanya boobz zipate support nzuri. Ukivaa the right pants, mfano umevaa tight dress alafu ukavaa seamless pants au bikini kwa casual dresses ..utakuwa mwenye kujiamini kwasababu unajua hakuna mistari inayochora on your booty.

 • Zinasaidia Kujenga Self Love

Maybe sio kweli kwamba haujipendi au haupendi mwili wako au sehemu ya mwili wako. Labda haujui tu namna ya kuweka asset zako sawa. Nina ndugu fulani wa mbali, kabarikiwa boobs. Miaka mingi alikuwa akilalamika sana, kifua kilikuwa kifua, alikichukia sana. Sikuona issue na the boobs ila yeye hakuwahi kuwa na amani nayo. Siku moja alibahatika kupata braa nzuri iliyomkaa vizuri sana. Zamani alikuwa anavaa hata bra mbili ili twins wakae sawa. Baada ya kupata hiyo braa aligundua kuwa kuna braa zinazoweza kufanya boobs zake zikae sawa na awe na amani. Aliamua kutenga pesa ili ainvest kwenye bra. Akashop bra kwa moyo mmoja, akajaribu, akazunguka maduka kadhaa mpaka akapata the right bra.

Bra zinazopush up bila kuwa na godoro ndani yak,siku hizi anajiita Nicki minaj. Hiyo ni nguvu ya the right undergarment. Mara nyingi tunajichambua na kujichanganua kwasababu tu miili yetu haifit katika nguo kama tunavyotaka japokuwa kuna namna ya kufanya zifit. Inawezekana ni kitambi kinalet down muonekano wote au ni nyama za kiunoni n.k Jibu lipo katika undergarment. Tafuta mavazi ya ndani yanayoweza kustiri mwili wako vyema.

 • Zinafanya Uonekane Sexy

Undergarment, hususani sahihi. Huwa na tabia ya kuminya na kuachia nyama za mwili pale zinapostahili kuminywa na kuachiwa. Kinachofanya mtu aonekane sexy or not ni body proportions, yani kiuno kionekane kidogo kuliko kifua na nyonga. Kingine kinachofanya mtu aonekane sexy ni namna alivyo smooth so vitu kama mapingili kiuoni na mabondebonde hufanya mtu ajisikie namna fulani.

Hakuna mtu ambaye hana mapingili kabisa, wala vinyama nyama au mabondebonde hata kidogo. The thing is, camera na apps zinajua sana kuficha hivi vitu na watu huvaa bodyshapers siku hizi. Ukiona watu kwenye social media usihisi kama vile you are less than them. Hatujakamilika, karibu kila mtu ana problem areas kwenye mwili zinazofanya asijione so sexy. Kuvaa the right undergarment husaidia kuweka kila kitu mahali pake na kufanya assets zipop vizuri.

 • Zinawezesha Kuvaa Mavazi Yenye Mitindo Migumu

Nimeongelea celebs na red carpet. Kinachofanya watu hawa wavae nguo ambazo wakati mwingine hauelewi inawezaje kufunika mwili ni undergarment sahihi. Unakuta gauni haina mikanda, mgongo wazi ila boobs ziko mahali pake. Sometimes inabidi ujue namna ya kutumia undergarment ulizonazo kwa ajili ya mavazi tofauti, stylist wengine hata huchana undergarment ili zifit nguo fulani.

Kuna kipindi beyonce alivaa tight iliyochanwa mguu mmoja. Wasanii wengi hunyanyua boobs kwa plasta kwasababu bra zina mikanda na unakuta nguo anayotaka kuvaa ni ya wazi sana so mikanda haipaswi kuonekana. Undergarment sahihi sio lazima iwe imenunuliwa hivyo, wakati mwingine jiongeze. Cha muhimu ikupe support nzuri na amani. Najua kuna wakati unashindwa kuvaa nguo fulani kwasababu nguo zako za ndani haziruhusu. Invest katika undergarment tofauti tofauti ili uwe na ya kuvaa katika kila vazi .

 • Kulipa Vazi Muonekano Bora Zaidi

Wakati mwingine unawaza outfit kichwani mwako na kwa mawazo yako hiyo outfit ni fire. Au unaenda kununua nguo, then kwa kuangalia tu unajua hii nguo moto. Haujaribu wala kujitazama kwenye kioo. Picha linaanza umeivaa utoke. Nguo haieleweki, sio mbele sio nyuma. Badala ya kupotezea nguo think twice. Shida ni nguo au ni namna inavyohang kwenye mwili wako. Kama issue ni mwili, Je undergarment nzuri itasaidia. Kama itasaidia then vaa undergarment sahihi kuisupport.

Kuna gauni nzuri ila nyama za kiuoni au kitambi kinafanya isikae sawa. Sometimes huitaji hata flat tummy ili nguo ipendeze zaidi. Maybe unahitaji tu nyama zijishindilie vizuri na mwili uonekane smooth ndani ya nguo. Sometimes rangi ya mikanda ya braa inaharibu muonekano so you need another bra. Kama unaweza kuboresha muonekano wa mwili then nguo itavutia zaidi.

 • Inakupa Uhuru Wa Kufanya Mambo Yako

Comfort is everything. Nguo ya ndani ikikaa sawa unajisikia amani. Amani katika kutembea, kunyanyua na kushusha mikono, kuinama, kujigeuza n.k Kwa mtu mnene, ukivaa gauni bila tights mapaja hujisugua na wakati mwingine kusababisha maumivu. Maumivu haya hunyima uhuru wa kutembea.

Ukivaa bra ndogo sana au kubwa sana, twins wanaweza kuamua wachomoke muda wowote so huwezi kuwa na uhuru. Ukivaa chupi ndogo sana utapata maumivu kwenye mapaja. Nguo yoyote ya ndani isiyo sahihi huondoa uhuru. Naposema undergarment sahihi namaanisha iwe na kitambaa , rangi, muundo na size sahihi. Kuna undergarments ambazo husaidia sana katika muonekano. Undergarments hizo huboresha sana muonekano wa mwili na nguo so jitahidi kuwekeza katika mavazi haya;

 • Bra Sahihi

Hakikisha una bra yenye size sahihi. Jifunze kuhusu size yako. Hakikisha una bra zinazokupa support vizuri. Mikanda ifit vizuri.For big boobs nunua zisizo na sponge na small boobs nunua zenye sponge. Bra zenye chuma kusaidia kunyanyia boobs vizuri. Nunua bra zenye mikanda na rangi mbalimbali. Buy some sexy bra for your babe, usimvalie ile bra nyeusi ya kila siku. Keep your bra clean.

 • Full Body Shappers

Body shapers huja kwa mitimdo mbalimbali. Nyingine huwa vest ya kubana nyama za mgongo, kiuno na tumbo. Nyingine hubana tumbo tu, nyingine hupitilizana kuwa na tights. Nyingine ni vest za kawaika. Mikanda ya tumbo hupunguza tumbo na kubana kiuno.

Hii hufanya hips kuonekana pana zaidi pia. Body shapers huwa na material mbalimbali. Nyingine hubana sana na nyingine kidogo. Chagua itakayokufaa zaidi na itakayokupa amani.

 • Bra Tapes

Kuna nguo huwezi kuvalia bra kabisa so kuna tapes za kubana boobs. Tapes hizi huwa za aina mbali mbali. Nyingine huwa kama bra zisizo na mikanda kabisa.

 • Tights

Tights ni muhimu, huzuia msuguano wa mapaja na kufanya mashimo kwenye mapaja yasionekane sana. Jitahidi kuwa na bra ndefu na fupi zenye rangi mbalimbali

 • Pants Za Mtukio Mbalimbali

Kuna.pants za kuvaa ukiwa period, siku za kawaida, kwa baby. Kuna pants za nguo mbalimbali. Nyingine hazina mikanda inayokata makalio ili uwe na amani uvaapo nguo zinazoshika. Nunua chupi zenye ubora na rangi nzuri. Ni vizuri kuwa na chupi nyingi na kuzinunia mara kwa mara.

Ni Matumaini Yetu Umejifunza Kitu,

Imeandikwa na @elegancebyRee

Related posts

4 Comments

 1. เซ็กซี่บาคาร่า

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-nguo-za-ndani-sahihi-katika-muonekano-wako/ […]

 2. brainsclub

  … [Trackback]

  […] There you can find 39123 more Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-nguo-za-ndani-sahihi-katika-muonekano-wako/ […]

 3. vigrx plus

  … [Trackback]

  […] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-nguo-za-ndani-sahihi-katika-muonekano-wako/ […]

 4. Fryd vape

  … [Trackback]

  […] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-nguo-za-ndani-sahihi-katika-muonekano-wako/ […]

Comments are closed.