SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Umuhimu wa Website kwa wabunifu
Mitindo

Umuhimu wa Website kwa wabunifu 

Ni wazi mitandao ya kijamii imeendeleza kufubaza akili za wabunifu wetu hata kuwafanya kusahau umuhimu wa wao na biashara zao kuwa na website.

Lakini mitandao ya kijamii pamoja na wingi wa watumiaje wake kamwe haitakuja kupoteza umuhimu wa website katika biashara. Ni wazi kupitia mitandao ya kijamii mbunifu anayonafasi kubwa ya kazi zake kuonwa na watu wengi ambao wanatumia mtandao husika, tofauti na website ambapo watu wakaotembelea ukurasa wako ni wale ambao wamedhamiria kweli kuona kile unachokifanya katika biashara yako, ikiwa ni pamoja na bidhaa zako.

Kwa kutumia mfano wa mkongwe Mustafa Hassanali tunaweza kuona tofauti ya website na social media. Picha juu ni muonekano wa website ya Mustafa Hassanali ambayo imepangiliwa vizuri ikiwa na vipengele vinavyoshibisha portifolio yake kama mbunifu. Ukitazama kwa makini utagundua website yake imejikita kwenye kazi yake tu, hii inawasaidia watu ama wateja wake wanapotaka kumfahamu vizuri mustafa, kwa kutembelea website yake tu utagundua yeye ni nani na anafanya nini kwenye tasnia ya mitindo nchini.

 

Lakini tukirejea kwenye mitandao ya kijamii, utagundua kuwa licha ya kuwa mbunifu mhairi pia anamaisha mengine nje ya jukwaa la mitindo ambayo tunapata kuyafahamu kupitia mitandao yake ya kijamii. Licha ya kuwa huwa anapost baadhi ya kazi zake, lakini hawezi kuweka picha zote, hii inaendelea kumtofautisha Mustafa wa Instagram na Mustafa wa kwenye website yake kibiashara.

Mfano huu mmoja utakupa mwangaza  juu ya umuhimu wa wewe kama mbunifu, stylist au model kutotegemea social media peke yake kwenye biashara yako. Ni vema kutumia social media kupeleka wateja kwenye website yako ambapo baadhi ya maswali ambayo watakuwa nayo kuhusiana na kazi zako wataweza kupata majibu yake huko.

Maswali yapo mengi ya kujiuliza, ikiwemo vipi kama wenye mtandao wao wakiamua kuufunga? wakati huo umetumia gharama nyingi kuwekeza kwenye mtandao husika na kujizolea followers wakutosha. Lakini hili haliwezi kutokea ikiwa unawebsite yako. Mtandao ukifungwa bado utakuwa na sehemu ya kuonesha kazi zako.

Sisemi msitumie mitandao ya kijamii kuweka kazi zenu, la hasha…ni vema ukatumia vyote ili kukuza chapa yako na biashara yako kwa ujumla.

Related posts

7 Comments

  1. see it here

    … [Trackback]

    […] Read More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-website-kwa-wabunifu/ […]

  2. Plantation Shutters

    … [Trackback]

    […] Read More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-website-kwa-wabunifu/ […]

  3. Buy Icarus Zoomies Edibles 3000mg In Canada

    … [Trackback]

    […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-website-kwa-wabunifu/ […]

  4. Study in Africa

    … [Trackback]

    […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-website-kwa-wabunifu/ […]

  5. 7 mushroom blend capsules

    … [Trackback]

    […] There you will find 55710 more Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-website-kwa-wabunifu/ […]

  6. alwero

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-website-kwa-wabunifu/ […]

  7. weed hotel delivery

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/umuhimu-wa-website-kwa-wabunifu/ […]

Comments are closed.