Vanessa Mdee A.K.A Vee Money anaweza kuchukua taji la mtu maarufu wa kike ambae amependeza sana mwaka huu, ikiwa tumesha ugawa mwaka mwezi huu Vanessa anaonekana kuwa ndio msanii wa kike anaye ongoza katika list yetu ya wanaopendeza leo tumeamua kumpa accolades zake kwa maana sisi tunapenda wale wasio tuangusha katika swala zima la mitindo.
Kwa mwaka huu vizuri ambavyo mpaka sasa tumeviona kutoka kwa Vee ni kwamba,
Anaweka effort katika mavazi yake, every little detail count’s kama ni mfuatiliaji utaona katika kila outfit lazima Vee aongezee kitu ambacho kitafanya vazi lake li-stand out, iwe kiatu, accessory au hata vazi lenyewe kama katika hizi outfit mbili
hii ya kwanza ambayo alivaa full black ameongezea na socks nyeupe ambazo zilifanya outfit yake i-pop lakini pia aliongezea accessories nyingine kama miwani na layered necklace’s, outfit ilikuwa casual yet fashionable.
Hapa alikuwa ameenda ku-perform Bukoba, alivaa outfit kutoka kwa mbunifu Chidy Designs tulipenda outfit lakini kilicho fanya hii outfit i-pop sana ni hizi accessories zake alizo ongezea hii miwani ya wire tupu bila kioo, fringe earrings na hii hair style yake kama ambavyo tulisema hapa juu every little detail count’s na Vee is serving us that.
Vee ana jaribu ku-keep up na fashion trends pia, 2018 umekua ni mwaka wa trends nyingi mbalimbali, Vanessa ameonekana kujaribu zile ambazo anaona zinaendana na mwili wake, style na uso wake. Trend ambazo tumeona akiwa amejaribu ni matrix sunglasses, Finger wave hair style na Off White Industrial Belt & tumependa jinsi ambavyo ameziweka zimeendana nae.
Kufikiria cha tofauti, Vanessa amekuwa akitupa style’s tofauti tofauti mara kwa mara hasa katika mitoko yake katika ku-perform jukwaani, lakini pia amekuwa akitumia wabunifu kutoka Tanzania katika mavazi yake kama hizi mbili ambazo tuliona amevaa hivi karibuni
sheer pieces kutoka kwa mbunifu Elisha Red label huku akiwa amemalizia na silver boots, zilizo match na outfit yake, petite
Na hapa akiwa amevaa red dress kutoka kwa mbunifu Kyamirwa, Lady In Red Vibes.
Talking about street style star in two pieces & see through plastic knee boots.
Well hiki ndio huwa tunamaanisha tukiwa tunasema wasanii wawe na star look na kuwa tofauti, ukimuangalia Vanessa ana styles za kipekee na sio muoga kujaribu, anatumia stylist na wabunifu katika kazi zake. Unapoingia katika account zake unapenda unacho kiona well Vanessa Deserves All the Accolades. Tuambie wewe unapenda styles za nani mwaka huu?
Related posts
4 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/vanessa-mdee-anamiliki-taji-la-fashionable-diva-mwaka-huu/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/vanessa-mdee-anamiliki-taji-la-fashionable-diva-mwaka-huu/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/vanessa-mdee-anamiliki-taji-la-fashionable-diva-mwaka-huu/ […]
… [Trackback]
[…] Here you can find 31083 more Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/vanessa-mdee-anamiliki-taji-la-fashionable-diva-mwaka-huu/ […]