SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Tips To Bounce Back After Having A Baby Inspired By Vanessa Mdee
Mitindo

Tips To Bounce Back After Having A Baby Inspired By Vanessa Mdee 

Vanessa is now mom of two, congratulations kwake na mumewe mwanamuzi Rotimi, well Vaness ana week kadhaa toka ajifungue na tunaweza kusema sis looks good, mwili wake upo vizuri ameongezeka lakini si sana.

Wengi wameonekana kusifia namna ameweza ku-bounce back baada ya kujifungua back to back, huku wengine wakijitoa kasoro kwamba wao wameshindwa kurudi katika miili yao baada ya kujifungua.

Well tungependa kuwakumbusha kwamba kwanza Vee ni mwembamba ni moja kati ya wale watu wana mwili mdogo kiasili, hajawahi kuwa mnene, tuseme hii ni mara ya kwanza kumuona Vee amegain hivi pretty sure yeye mwenyewe anajiona kibonge wakati sisi tunamuona kawaida. Kwaio kama wewe mwili wako wa asili ni mnene usijifananishe na Vee.

Kunyonyesha inavyosemakana ukinyonyesha mwanao basi una burn calories, hivyo kama umejifungua na bado una nyonyesha jitahidi usimuachishe mtoto nyonyo mapema ili apunguze hizo mafuta mwilini.

Vee hanywi mitori, kwetu ukijifungua ni mwendo wa mitori, mavyakula yenye kunenepesha tofauti na ukiwa kwa wenzetu, tunauhakika Vee hata kama anainywa mitori basi ni mara chache sio kila siku, incase unamtoto mchanga au mjamzito weka hili kichwani kama inawezekana ukapunguza au ukinywa ujitahidi na kufanya mazoezi.

Fanya Mazoezi, wakina mama tunajua tunachoka baada ya kujifungua, jipe muda kama week au week mbili kupumzika baada ya hapo jitahidi kufanya mazoezi madogo madogo sio tu yatakufanya mwili upungue bali pia kurudisha mwili katika hali yake ya kawaida, kukufanya muscles zikaze na kuwa na nguvu, mazoezi yanakupa enery, utalala vizuri lakini pia kukusaidia kupunguza stress.

Well usiwaze sana kuhusu mwili pia furahi umepata bundle of joy.

Related posts