Hello Afromates ni jumanne nyingine tena ambayo huwa tunawaletea habari kuhusu viatu, iwe nani amevevivaa, bei yake au kwanini you should own that pair of shoes, Jumanne ya leo tunawaletea viatu vya Louis Vuitton ambavyo tumeona watu maarufu mbalimbali kutoka Tanzania na Kenya wakivivaa. Hizi ni ankle boots ambapo tulisha wahi kuandikia umuhimu wa mtu yoyote kuwa na viatu aina ya boots.

Long story short tumeona sasa hivi watu maarufu wengi wakivaa boots tumemuona Hamisa Mobetto, Amber Lulu na wengine wengi lakini ambavyo tumeona kidogo vimejirudia ni hizi LV ankle boots.

Tumemuona our 2018 fashionable celebrity of the year Vanessa Mdee akiwa amevalia boots hizi na all black outfit akiwa amevalia na bag belt ya Lv kiunoni akamalizia na layered necklaces na miwani, she looked dope.

Kama viatu hivi ni Original basi itakuwa amenunua kwa Eur 870 sawa na Shilingi za ki-Tanzania 2,279,044.64.

Mwanamuziki kutoka Kenya, Victoria Kimani yeye alivaa Lv Star trail Ankle Boots na two pieces outfit ambazo ni biker shorts nyeusi na clop top nyeusi akiwa amemalizia na long denim jacket na extra beret, akiwa ameongeza rangi katika muonekano wake na neon yellow color na red makeup, how extra is her casual outfit look?

Katika website ya Louis Vuitton viatu hivi vinauzwa Eur 970 sawa na shilingi za ki-Tanzania  2,541,019.06

Muigizaji na fashion influencer Irene Uwoya yeye alionekana aliwa amevalia viatu hivi na laceup cream leggings, spaghetti strap top nyeusi na akiwa amemalizia muonekano wake na Lv handbag na miwani, so hot Irene is a vibe these days

kama macho yetu yatakuwa hayatudanganyi viatu vya Irene vinafanana na vya Victoria na kama ni kweli basi viatu hivi vinauzwa bei sawa na vya Victoria Kimani ambapo ni Eur 970 sawa na shilingi 2,541,019.06 za Ki-Tanzania kama ni original kutoka kwa Lv wenyewe.

Well Afromates unadhani nani kavitendea haki viatu hivi?

Comments

comments