SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Vifungo Vinavyoweza Kupunguza Hadhi Ya Vazi Lako
Mitindo

Vifungo Vinavyoweza Kupunguza Hadhi Ya Vazi Lako 

Kuna vitu vidogo ambavyo unaweza kupuuzia na kusema havionekani au hata kama vinaonekana sio big deal lakini kiukweli vinaweza kutoa muonekano wako kutoka 100% to 70% kitu ambacho kinakera maana umechukua muda mwingi kufikiria mtoko wako halafu kitu kidogo tu kina uharibu.

  • Je unajua vifungo vinaweza kufanya vazi lako lionekane cheap?

Utajiuliza vifungo vinawezaje kufanya vazi lionekane cheap? Kifungo ni kitu ambacho ni rahisi kuwa noticed, vifungo vipo mbele kabisa kama sura hivyo ni rahisi kuonekana kwa haraka.

Namna gani vifungo vinaweza kupunguza hadhi ya vazi lako?

  • Kifungo kimeshonwa na uzi rangi tofauti

Unakuta labda kifungo kilichomoka ukaamua kukishona mwenyewe na kwa bahati mbaya hukuwa na uzi unaoendana rangi na vifungo vingine, hii inapunguza u-smart wa vazi lako linaonekana lina dosari hakikisha kama umekosa uzi unaofanana na vifungo vingine basi subiri hadi uupate au shona vifungo vyote kwa rangi ya uzi uliyonayo.

  • Kifungo kuwa rangi tofauti na vingine

kama tulivyoongelea kwenye uzi inaweza ikawa kifungo kilichomoka na hukikiona, unakuja kushtuka kimeshapotea unaamua kutafuta kingine chochote unashonea, una haribu show ya vazi lako, kama umeshindwa kupata kinachoendana na vilivyobaki basi shonea vyote kwa vile ambavyo unavyo ili usiweke dosari kwenye vazi lako.

  • Vifungo vinavyo ng’aa sana

Umenunua vazi ukakuta vifungo vina scream yaani unaweza kukuta vina rangi fulani inakelele au rangi ni gold lakini ile cheap gold, inasababisha vazi lako kuoneka cheap, badilisha vifungo hivyo na tumia vyenye rangi iliyotulia na inayoendana rangi na vazi lako.

Ni matumaini yetu umejifunza kitu, tuambie ni kosa lipi kati tuliyo yataja umeshawahi ku-commit?

Related posts