Kuna baadhi ya vitu ambavyo jamii imejiwekea ni vya kike na vingine vya kiume, kuna uzi mwembamba ambao unatakiwa usivukwe lakini kama ambavyo wazee wazamani walisema “Sheria zimewekwa ili zivunjwe”. Karne ya sasa hivi hakuna hio mipaka sasa hivi kila mtu yupo free kufanya anacho kitaka tunaita Unisex Style.
Ilikuwa si hali ya kawaida kumuona mtoto wa kiume akiwa amevaa skirt, kuvaa kikuku, kutoboa pua, masikio au hata kusuka kwa sababu ilikuwa ikiaminika ni vitu vinavyopaswa kufanywa na wanawake.
Tunakumbuka vizuri miaka kadhaa nyuma mwanamuziki wa Hiphop Chidi Benz alitoboa pua na watu walimrushia maneno ya hovyo sana lakini yeye alisema
“kila kitu ni mtu jinsi unavyoishi, mimi nilitoboa pua mara ya kwanza nilivyosafiri nikaacha pini kwa hiyo ikaziba kidogo kwa hiyo nilivyorudi nikaenda kutoboa tena, hizi ni hisia zangu na vitu vyangu nilivyoviona kwenye macho yangu pamoja na mimi mwenyewe ninavyoishi vitu vilivyonipitia binafsi mimi binafsi kama Rasheed nikajikuta siku tu nimeamka nikaenda town nikajitoboa nikalipa pesa nikarudi nyumbani baadae ndio nikagundua hivi nimetoboa pua.

”Chidi aliongezea kwa kusema “ni alama ambayo nimeiweka kama ni maumivu basi nitayakumbuka yale maumivu na nisiumie tena, kama ni furaha basi nikumbuke ile furaha.. kwa hiyo mimi ndio ninaelewa, nashindwa kuelewa kama kuna watu wanachukulia tofauti kwa sababu unashangaa nini kutoboa pua na nikitoa pini pua inaziba kama kawaida, nini inasababisha uanamke au u**** kwa kutoboa pua, ukiamua unaamua tu kuna watu maaskari bwana na wanajeshi na watu wanasema huyo hivi na yule hivi kwa hiyo kwa kuongea kwako ovyo ntakushtaki kwa sababu itaziba na hutoniambia kitu unajua.”
Lakini tukaja kumuona msanii mwingine mkubwa, Diamond Platnumz na yeye akiwa amevaa kipini puani, na yeye hakuachwa na mashabiki na wale ambao sio mashabiki kwa kufanya kitendo hiko

Kwa sasa tunamuona msanii wa R&B Damian Soul yeye akiwa anavalia nose ring, hii imetufanya tuwaze je ni sawa kwa mwanaume kuvaa nose ring au kutoboa pua? Na nini ambacho kinafanya mwanaume kutoa pua au kuvaa baadhi ya vitu kukatazwe au kuonekana ni kinyume na maadali ya jamii?
Kama pua anayo na ni urembo kwa ajili ya pua ni nini kinasababisha mwanaume akivaa apigwe mawe?

Tukumbuke hawa sio wanaume wa kwanza au wasanii wa kwanza wa kiume kuvaa vidani vya pua, mwanamuziki 2 Pac kabla ya umauti wake alitoa pua na kuvaa kipini,

Lakini pia mwanamuziki Chris Brown pia huwa unavaa kipini puani mara kwa mara

Inasemekana kwamba baadhi ya wanaume wanaovaa vipini puani wanapendeza mno, swali letu kwenu je utamuachia rafiki, mpenzi au ndugu yako wa kiume avae kipini puani? Na kwanini?
Related posts
6 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/vipi-kuhusu-wanaume-kuvaa-kipini-puani/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/vipi-kuhusu-wanaume-kuvaa-kipini-puani/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/vipi-kuhusu-wanaume-kuvaa-kipini-puani/ […]
… [Trackback]
[…] Read More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/vipi-kuhusu-wanaume-kuvaa-kipini-puani/ […]
… [Trackback]
[…] There you can find 25538 more Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/vipi-kuhusu-wanaume-kuvaa-kipini-puani/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/vipi-kuhusu-wanaume-kuvaa-kipini-puani/ […]