SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Vitu Vitano Unavyoweza Kufanya Ku-level Up
AfroTipAndTricks

Vitu Vitano Unavyoweza Kufanya Ku-level Up 

Najua wengi wetu tumeenda shule kuna wale wadada ulisoma nao, wakati unasoma nao walikuwa the true definition of basic. Ukimuona hakutetemeshi hakutishi(wasemavyo waswahili). Basi umemaliza shule, miaka kadhaa imepita then katika pitapita zako unakutana nae au unaona picha yake mtandaoni, wakati mwingine hata rafiki anakutumia picha yake na kitext kama hiki, ’’Eti huyu ni Fulani,’’ alafu wewe unamjibu kwa emoji za mshangao. Muonekano wa huyu mtu ni tofaui kabisa she isr from basic, beyond your average chic. Unaweza kusema ni mtu tofauti, siri katika transformation hii iko katika vitu  vitano. Mara nyingi mabadiliko huchochewa na vitu vingi; Kuna kuachwa na kiboyfriend hahaa, Kuwa inspired na mwanamke mwingine, Kubadili mazingira, kuongeza kipato, Kupata self esteem and self confidence, Kujipenda Zaidi n.k. So pamoja na kuwepo na sababu mbalimbali za kuleta transformation ya mwili kuna sababu  nyingine ambayo ni ya muhimu Zaidi, KUFANYA MAAMUZI. Yes! Kufanya maamuzi. Like hauwezi kukaa unasubiri external factors zikupe a glow up and hauhitaji kuwa na kipato kikubwa kuglow up japo pesa itatumika na kiasi kitakachotumika ni maamuzi yako. Twende kwenye vitu hivi vitano;

BODY (SHEPU, UZITO)

Kitu kitakachobadilisha muonekano wako na kukupa the biggest glow up of your life ni kuboresha muonekano wa mwili wako. Kama ulikuwa so slim unaweza kuongeza uzito na kama uko overweight punguza uzito. Kujithamini hivyo ulivyo ni kitu kizuri sana na kama umeridhika na hilo basi good for you but kwa warembo wanaotaka kuglow up, kuboresha muonekano wa mwili kutabadilisha image yako kabisa. Ofcourse sio rahisi, nothing worth having huja kirahisi. Lazima uwe na nia na nia iambatane na matendo lakini matokeo yake ni worth all the sacrifice. Naona watu wengi wanahisi hawawezi kubadili muonekano wa mwili kwasababu ya mentality, kila siku unajiimbia mimi siwezi kupungua kwakweli…uumm hautopunguza sweery! sio kwa mawazo hayo. I help women improve their bodies by improving their mentality first, DM me baby. Kuna wale wameridhika na uzito ila mazoezi kadhaa yatafanya body iwe kinanda so do something kuboresha muonekano wako.

NGOZI

Niliwahi kusoma na mdada A level alikuwa na chunusi nyingi sana, sehemu nyingi za sura yake zilikuwa na makovu meusi yaliyotokana na zile chunusi. Nilikuja kuonana nae tena nikiwa nimemaliza chuo. My goodness siku nimemuona, I was like wow! Ngozi kama ya mtoto, kanizidi na mimi ambaye sikuwa na chunusi. She was so soft, baka moja tu lililokuwa linafifia, ngozi imeng’aa  ina nuru. Hakuwa na kitu cha ajabu kingine mbali na ngozi ila ile ngozi ilimbadilisha kabisa. Alionekana wa tofauti, her face was prettier and alionekana mwenye nuru na furaha. Ladies, take care of your skin. Ngozi nzuri huboresha hata muonekano wa makeup. Inaboost confidence na kukufanya uvutie Zaidi. Unaweza kuboresha muonekano wa ngozi kwa kufanya exfoliation, kutumia product za kuongeza mng’ao na nuru kama African black soap, shea butter na nyingine za madukani. Kama una madoa au chunusi weka jitihada katika kuzitoa. Kuna watu akijaribu product moja ikafeli ndio basi tena, akijaribu product asione matokeo ndani ya siku tatu anarukia nyingine. Pia tunakuwa wavivu kufanya research wakati tuko katika miaka ambayo taarifa zipo kila kona. Please google naah!(In Nigerian accent)

MAVAZI

This is the holy grail, Mavazi ni CV. Mavazi yanakutambulisha kabla hujatamka neno. Mavazi yanaweza kusema this here is a boss woman, maana halisi ya kujiamini, malkia katika ulimwengu wake, mdada wa nguvu. Mavazi hayohayo yanaweza kusema huyu kashajikatia tamaa ya maisha, yeye chochote twende tu, kunyoosha nguo ndio kitu gani? Unaona! Kitu ambacho unaweza usikitilie maanani kina nafasi kubwa sana. Usiniquote vibaya hapa, sijasema kabisa gharama ya nguo bali mavazi tu. Katika mavazi kuna unavaa nini, unavaa wapi, unavalia nini, unajiskia vipi ukivaa hivyo? The moment ukiamua kuvaa kwa ajili ya mwili wako, kufanya majaribio ya rangi zinazokupendeza (Mimi binafsi naona nikivaa nguo zenye bright colors ninasifiwa kuwa nimependeza), kununua kwa ajili ya ubora na sio wingi na kujifunza uvae nini na nini then wewe ni mtu tofauti. Hauhitaji kuwa mtu mwingine au kuvaa kama Fulani, dress like you but iwe better tu.

QUALITY

Hapa ndipo wengi hufeli. Ili kujua kama upo kwenye hili kundi jiulize maswali haya

  • Una nguo ambazo unapitisha Zaidi ya miezi mitatu bila kuzivaa lakini hukuzinunua muda mrefu sana?
  • Kuna kipindi unakosa nguo za tukio fulani mfano beach, harusi, lunch date unaamua uvae chochote tu?
  • Una nguo nyingi hazina mwaka lakini muonekano wake hauvutii
  • Una nguo ambazo ulinunua mwenyewe kwa pesa yako ila haujui utava lini wala wapi, yani huna pa kuivalia.
  • Una nguo nyingi sana ila ukiambiwa jiandae unakesha kutafuta cha kuvaa?

Hizi ni dalili kuwa haununui kwa ajili ya ubora bali wingi. Kama unaona ni bora uwe na nywele za plastic kumi badala ya human hair moja au mbili, kama Ni bora uwe na viatu vya bei ndogo vingi badala ya pair chache za maana, kama ni bora ukasagule viwalo vingi kwa elfu 30 badala ya kununua classy dress moja hata ya mtumba na wewe uko kwenye hili kundi.

Kinachotucost ni kutokuwa na budget, hakuna plan za mavazi, haujichambui na kujichanganua kuwa unapenda nini na unataka nini katika uvaaji. Akili iko on autopilot so we just buy and buy and buy. Pia hatuna uvumilivu wala utamaduni wa kusave hela kwa ajili ya kitu fulani so tunanunua tu baada ya miezi kadhaa huwezi kuvaa tena ulichokinunua. Mimi binafsi nimekuwa member wa kundi hili, nilikuwa nanunua tu vitu kwasababu viko trendy, au nina hela, au nimekitamani tu baada ya muda I’m like mmmhh this is not my style kwakweli na anaefaidika ni mdogo wangu. Kama unapata shida katika hili, I am here to help. Follow me at elegancebyree instagram.

Jitahidi kununua vitu kwa ajili ya ubora na namna vitakavyoboresha muonekano wako. Ubora uwe katika rangi, kitambaa, Style, muonekano, Kuwa na sehemu na nguo nyingine za kuvalia n.k. Kama kabati yako imejaa quality then you will look like a quality queen.

KUJIAMINI (BODY LANGUAGE)

A woman’s best outfit is not her smile, but you should smile baby. A woman’s best outfit ni kujiamini. Feeling like, walking like and talking like a damn queen that you are. Kuna watu hawaglow sana but confidence inafanya wavutie Zaidi. That kajifeeling ka kuwa confident in your entire being…your skin…your body and ofcourse your mind hufanya mtu aonekane sexy tu. Na simaanishi kiherehere tafadhari , but kuwa nacho it’s good…mi ninacho and ukinifollow instagram at elegancebyree then utafahamu umuhimu wa kiherehere. When you feel good about yourself hiyo energy huonekana hata nje. How you pose  inakuwa tofauti, nguo unazochagua na unazovaa zinakuwa better, you take better care of yourself. Improve muonekano wako lakini cha muhimu fanya the inner work kuhakikisha unaongeza kujiamini kwako na fahamu kuwa kujiamini hutokana na kujithamini na kujipenda yani self love and self esteem. Namna mojawapo ya kufanya hivi ni kwa kusoma vitabu na kutazama content katika media mbalimbali kuhusiana na hili na pia kuwa na mentor wa kukusaidia na kukupush kufikia malengo haya. I can help you gain confidence and self love kupitia  course yangu ya ‘I AM A QUEEN’ fanya kunifollow na kunidm kama uko interested. 

Napenda kuona wadada wakijipenda na kujithamini Zaidi na kufikia ndoto zao. Kama unapenda pia fanya kushare na warembo unaowapenda na kuwathamini. Mrembo kama mtu kashare hii aricle na wewe, that person loves baby girl.

Imeandikwa na @elegancebyRee

Related posts