Ukiwa mwaka ndio unaelekea kuisha imetubidi tupitie vipengele mbalimbali vya mitindo, leo tumepitia kwa wabunifu wanao chipukia na ambao tunadhani wakiendelea hivi mwaka 2016 wanaweza kufanya mwakubwa katika ulimwengu huu. Wapo wengi na inawezekana wengine hatuja waona ila kati ya wengi tulio waona hawa wame tuvutia zaidi kutokana na kazi zao na hasa ni kwamba bado hawajatoka je? wakitoka watafanya makubwa kiasi gani
Lilian Ndanshau au @liliandanshau
Kazi yake ya kwanza kuiona ilikua scetch/mchoro wa kazi yake alio kuwa kauchora kwa ajili ya shindano la Fasdo ikabidi tumtafute na tuone ni nini hasa ana fanya, Lily ukiachana na ule mchoro tu kutuvutia baada ya kutembelea ukurasa wake tukagundua ana kipaji cha aina yake hasa kwenye umaridadi wa mitindo yake ana pangilia rangi na ni msafi kazi yake huwezi kuamini kama ni msichana mdogo tu.
Yvette Nicole Nkhoma au @two_in_one_accessories
Yvette ana tengeneza vito/urembo wa aina mbalimbali mara ya kwanza kumuona hatukudhani kama ni mtanzania lakini baadae tuka gundua ni mtanzania na ni msichana ambae anajua nini ana fanya na hafanyi kitu kwa sababu tu ana fanya ila hufanya kile anacho fanya kwa uhakika
Mgombelwa au @mgombelwabrand
Ni kijana mdogo kutoka morogoro ambae ana buni mavazi ya kiume mara ya kwanza kumuona ilikua katika sanaa fashion show ambapo tuli tabiri hata ishia hapo na kweli tukaja kumuona pia peroni Tanzania fashion nite lakini pia tuna tabiri hata ishia hapa na jicho letu lipo kwake mwaka 2016
Florinya au @frolinyadesigns
Ni mdada mwenye kipaji cha pekee yeye hutumia uzi wa kushonea vitambaa vya nyumbani kushonea urembo kama herene,mikufu hata vivazi vya watoto. Florinya ana fanya kazi nzuri mno na ina vutia hasa machoni kwa watu pia tunahisi mwaka 2016 ana fanya makubwa zaidi
Manyatta au @manyatta_101
Manyatta wana fanya urembo pia nao tuna hisi 2016 wata fanya makubwa zaidi
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…