SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Wateja Wanachangia Kudumisha Sekta Ya Mitindo Nchini
Mitindo

Wateja Wanachangia Kudumisha Sekta Ya Mitindo Nchini 

Imekuwa kawaida yetu kuchukua muda kutafuta nini kinakwamisha Tasnia ya mitindo Nchini na nini kifanyike ili kuondoa changamoto hizi zinazosababisha kudorora kwa sekta hii mahsusi duniani kote. Mara nyingi tumekuwa tukilalamikia stylists na wabunifu kuhusu kukosa ubunifu na upekee katika kazi zao, wabunifu wanacopy (kunakili) kutoka kwa wabunifu wengine, stylists kadhalika style zao ni zilezile kila siku.

Tumejiuliza swali, je nini kifanyike? Kwanini sisi ni watu wa-kucopy tu? yaani kila unapoona design (mtindo) fulani nzuri basi unakuta kumbe imeibiwa mahala fulani kwa aidha mbunifu mdogo au mashuhuri. Tafakari yetu ikaturudisha nyuma kidogo katika kupembua changamoto hii ambayo imezidi kukuwa katika sanaa ya ubunifu wa mavazi. Katika kutafuta majawabu ya nini hasa kinachangia, Afroswagga ikafanya kautafiti kadogo ambako kamewamulika wateja kama chanzo kikubwa cha kudumaa kwa sanaa hii. Licha ya kuwepo kwa kudumaa kwa ubunifu katika sanaa ya ubunifu, lakini pia wateja wamekuwa na influence (ushawishi) mkubwa katika kuwafanya wabunifu watu washindwe kutoka nje ya comfort zones zao.

Kwa wateja kisanga kinakuja pale mteja anapoenda na mtindo wake kichwani badala ya kumuachia mbunifu kufanya kazi yake. Jamani unapokwenda kwa stylist au mbunifu kutaka service (huduma) unatakiwa umuachie na kumuamini afanye kazi yake. Lakini unapoenda na idea yako hapo huitaji service ya stylist wala mbunifu bali unataka service ya personal shopper na fundi cherehani. Yes personal shopper yeye kazi yake kukununulia mavazi ambayo wewe unayataka wakati stylist yeye kazi yake yeye ni ku-coordinate mavazi ya mteja wake. Na kwa mbunifu kazi yake ni kukubunia vazi wakati fundi cherehani (mshona nguo) yeye kushona ile ambayo imeshabuniwa.

Tunadhani hii inachangia kwa kiasi kikubwa Tasnia yetu kuzorota, inawezekana wabunifu wanajua kubuni na stylist wanajua ku-style lakini hawawezi kwenda kinyume na matakwa ya wateja wao. Tungependa muwaachie wafanye kazi zao, kama umeona kazi yake ukaipenda mpaka ukaamua kumtafuta ni vyema ukamuacha aifanye hio kazi yako kwa namna ambavyo yeye anaweza, hii sio tu itamsaidia mbunifu kuonekana anajua nini anafanya bali pia kukupa wewe muonekano wa tofauti na pia kazi zetu kuonekana kwingine.

Wateja pia huridhika, mfano mara nyingi sisi huwa tunapost wabunifu ambao wamechukua ubunifu kwa mtu mwingine ukisoma comment kwenye post za hizo picha utagundua asilimia kubwa hatuna uelewa wa ubunifu, wengi wanamsifia mbunifu amefanya kazi nzuri kuliko mwenye kazi yake, well yes lazima aifanye vizuri maana kashakuta imeundwa. Yeye anaifanyia marekebisho machache anaiachia huko nje. Tunasahau yule ambae alituliza kichwa chake akabuni kuanzia chini.

Pale ambapo mteja anapo sema ni sawa mbunifu ku-copy mbunifu mwingine sababu hamna cha ajabu vyote vimesha fanywa inatufanya tuwaze, “inakuaje wabunifu wa wenzetu wanafanya kazi zinatoka zikiwa zina extra touch’s halafu sisi tunasema vyote vilisha fanywa?” Ni kweli skirt haiwezi kubadilika itaitwa skirt au gauni lakini ni nini unaongezea katika hilo vazi ndicho kinacho matter na kuitwa ubunifu.

Licha ya wateja kuwa chanzo cha kucopy kwa kazi za watu, lakini mwarobaini wa tatizo hili ni pale tu mbunifu atakapo anza kutoa collection zake mwenyewe ambazo ni kwa ajili ya kuonesha wateja uwezo wake. Tunajua changamoto ya wabunifu wengi kushindwa kutengeneza collections zao ambazo zimekuwa zimebuniwa kwa ajili ya kushowcase ni mtaji, lakini taratibu tutafika. Sio lazima uanze na collection ya nguo 10 au 20. Anza na ulichonacho, waache wateja waone uwezo wako jinsi unavyoweza kubuni na kudesign mtindo mbalimbali ambayo wanaweza kuvaa.

Related posts

5 Comments

 1. Elon Musk and how he became a USA citizen

  … [Trackback]

  […] Here you can find 92701 additional Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/wateja-wanachangia-kudumisha-sekta-ya-mitindo-nchini/ […]

 2. Darknet market links 2023 thank You!

  … [Trackback]

  […] There you will find 51214 additional Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/wateja-wanachangia-kudumisha-sekta-ya-mitindo-nchini/ […]

 3. buy ephedra sinica

  … [Trackback]

  […] There you will find 74338 more Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/wateja-wanachangia-kudumisha-sekta-ya-mitindo-nchini/ […]

 4. 호두코믹스

  … [Trackback]

  […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/wateja-wanachangia-kudumisha-sekta-ya-mitindo-nchini/ […]

 5. สล็อต ฝากถอน true wallet เว็บตรง 888pg

  … [Trackback]

  […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/wateja-wanachangia-kudumisha-sekta-ya-mitindo-nchini/ […]

Comments are closed.