Ikiwa leo ni jumatano nyingine ambayo kama utapitia mitandaoni utakuta zime postiwa picha nyingi za wana wake na chini zime andikwa #WCW, WCW maana yake ni Woman Crush Wednesday ambapo wengi huwaweka wale wanawake wawapendao eidha ni familia, rafiki, au watu maarufu wanawake lakini je tunajifunza nini kutoka kwa hao watu? Leo sisi Tuna WCW watano ambao ni wanawake sita kutoka Tanzania wanao jihusisha na maswala ya mitindo na wana kampuni zao binafsi
SHEKHA MANJANO, Mmiliki wa shear Illusion na Luv Touch Manjano
Shekha ana miliki kampuni ya Luv Touch Manjano ambayo ina bidhaa mbalimbali za urembo ikiwemo powder, Lipstick na vingine vingi ukiachana na kumiliki kampuni hio shekha ana toa ajira kwa kina mama kwa kuwapa mafunzo ya kupaka make up ili waweze kujiajiri wenyewe.
TAUSI LIKOKOLA,
ni mwanamitindo wa kimataifa ambae kwa sasa ame pumzika kazi hiyo Tausi ni mmiliki wa TAUSI DREAMS na pia ana bidhaa za nywele, Tausi pia ni #WCW wetu kwa leo kwa sababu ana jituma lakini pia ametoa ajira kwa wanawake wengine.
WEMA SEPETU, Miss Tanzania 2006 na mmliki wa Kiss by Wema Sepetu
Wema Sepetu ni muigizaji lakini pia alishawahi kuwa Miss Tanzania kwa sasa Wema anamiliki Lipstick ziitwazo Kiss By Wema Sepetu, ana faa kuwa WCW kwa kazi nzuri anayo ifanya.
JOKATE MWEGELO Miss Tanzania (namba mbili) 2016 na mmiliki wa Kidoti Hair na sandals
ukiongelea wadada wanao jituma Tanzania basi huwezi kuacha kumtaja Jokate ana miliki bidhaa za kidoti ambazo ni sandals na nywele, Jokate ni mwanadada anae jituma lakini pia ametoa ajira kwa wasichana wengine.
Flaviana Matata Mwanamitindo wa kimataifa na mmiliki wa Lavy Nail Polish
Flaviana Matata ni mwanamitindo kutoka Tanzania ambae kwa sasa yupo kimataifa zaidi ana fanya kazi zake na makampuni mbalimbali nje ya nchi Flaviana hivi karibuni amezindua rangi za kucha ambazo ni bidhaa zake zinazo enda kwa jina la lavy.
NASREEN KARIM Miss Tanzania 2008 ambae ana miliki bidhaa za ENJIPAI
Nasreen ni Miss Tanzania 2008 ambae ana miliki bidhaa za enjipai urembo wa kimasai, Nasreen ameweza kutoa ajira kwa kina mama wa kimasai na wakina mama wengine kutokana na bidhaa zake hizo.
Related posts
4 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] There you will find 69923 additional Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/wcw-tunajifunza-nini-kutoka-kwao/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/wcw-tunajifunza-nini-kutoka-kwao/ […]
… [Trackback]
[…] There you will find 90905 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/wcw-tunajifunza-nini-kutoka-kwao/ […]
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/wcw-tunajifunza-nini-kutoka-kwao/ […]