Ikiwa ni Jumatano nyingine ya mwaka 2016, tunakuletea WCW (Woman Crush Wednesday) tunakuletea wanawake ambao wametumia vipaji vyao kujiajiri na wanailetea Nchi yetu Sifa nzuri, wanawake hawa wote wanne ni wanamitindo kutoka hapa Tanzania lakini pia wanme vuka nje ya Nchi na kufanya kazi na makampuni makubwa ya huko.
Flaviana Matata.
ni mwanamitindo kutoka Tanzania amabe alianza kama miss universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana ameweza kufanya kazi na kampuni kama WILHELMINA (NYC,Miami,LA & London) NEXT MODELS (Paris & Milan) BOSS MODELS (South Africa). Ana Foundation amabayo inasaidia watoto wa kike kiElimu na pia ameanza ujasiriamali wa kuuza rangi za kucha ambazo ni za kwake mwenyewe.
Herrieth Paul.
Pia ni mTanzania nae mwanamitindo ambae kwa sasa anaiwakilisha Tanzania vyema zaidi, Herrieth ana miaka 20 tu na ameweza kufanya kazi na wabunifu wakubwa kama Diane von Fürstenberg, Lacoste, Tom Ford, Calvin Klein, Armani, Cavalli na 3.1 Phillip Lim, na hivi karibuni Herrith ametajwa kuwa sura mpya ya vipodozi vya maybelline.
Hapiness Millen Magesse
aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2001 ambapo pia aliwaikilisha Tanzania katika Miss World mwaka huo huo, baada ya hapo Hapiness alihamia South Africa kufanya kazi zake ambapo alikuwa mwanamitindo wa kwanza kutoka Tanzania kusainiwa na kampuni kubwa ya Ford Modelling, Hapiness pia ana Foundation yake inayo saidia wanawake wanao sumbuliwa na Endometriosis ugonjwa ambao na yeye unamsumbua kutokana na kazi yake hiyo Hapiness ameshinda Tuzo ya ‘Global Good Award‘ mwaka jana.
Tausi Likokola.
Tausi Likokola ni mwanamitindo ambae ame staafu kwa sasa, tausi amewahi kufanya kazi na wabunifu wakubwa kama as Gucci, Christian Dior, Tommy Hilfiger, Issey Miyake na Escada Tausi amefanya kazi pia na magazeti makubwa duniani, ukiachana na kazi hio Tausi ana kampuni yake ya nywele na perfume ambazo pia ameajiri wa Tanzania, Tausi ni mwandishi na ana NGO ambayo inasaidia Kuimarisha Elimu na Afya.
Related posts
5 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/wcws-flaviana-matata-millen-magesse-tausi-likokola-herrieth-paul/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/wcws-flaviana-matata-millen-magesse-tausi-likokola-herrieth-paul/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/wcws-flaviana-matata-millen-magesse-tausi-likokola-herrieth-paul/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/wcws-flaviana-matata-millen-magesse-tausi-likokola-herrieth-paul/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/wcws-flaviana-matata-millen-magesse-tausi-likokola-herrieth-paul/ […]