Jana katika Birthday Party yake, Wema Sepetu alizindua Lipstic alizo lipa jina KISS, Lipstick hizi ni bidhaa zake mwenyewe Wema. huwa ina semwa tafuta katika miaka ya 20-30 ili ule matunda katika miaka yako ya 40, hiki ndicho anacho kifanya wema sasa.
Katika Kurasa ya mtandao wa instagram mmoja wa washirika walio shirikiana na Wema mpaka kufanikisha jambo hili Mr problem solved aliandika yafuatayo kuhusiana na bidhaa hii,
#KissByWemaSepetu is here! Wakati habari zinaendelea kusambaa mtandaoni, ningependa kufafanua vitu mbali mbali:
1) Wazo la kutengeneza hivi vipodozi ni la Wema mwenyewe. Akishirikiana na kaka meneja, walibuni jina la KISS, wakachagua rangi, design ya box unalaliona kwenye picha, na hadi kupata kiwanda cha kuzitengeneza.
2) Kazi ya kusimamia safari ya vipodozi kutoka kiwandani hadi mikononi mwenu ndio kazi yangu. Kuna mambo mengi hapo kati kama kufatilia usajili kule TFDA, kuandaa duka, kuajiri wafanyakazi wa dukani, kupiga mahesabu ya bei, kuweka mfumo wa kisasa wa kuuzia pale dukani (yani Minishop System), nk. Maongezi mengi na marefu kuhusu mbinu ya biashara hii kwa ujumla nimefanya na rafiki yangu @wemadaily ambae kama mimi, anakua macho usiku wa manane kwa mwendo wa Team Popoozzzzz.
3) Vipodozi vya Wema vinapatikana DUKANI KWA WEMA TU! Hamna mawakala, na hamna sehemu nyingine yoyote ile yakuvipata. USIINGIZWE MJINI NA MATAPELI, ukauziwa madude feki yakakuharibu sura bure!
4) Bei ya lipstick na lipgloss ni elfu 40 ile ile, kwa piece moja. Hizi picha zenye kibox hicho ni za maonyesho tu, huwezi kuuziwa kibox kizima wala hatuuzi kwa seti (ingawa unaweza kuchagua moja moja kutoka kwenye rangi zote, ukauziwa bila shida)
5) Tumepanga kuvipeleka dukani kuanzia Jumatano hii, tarehe 4 November. Nategemea Wema atakuja, ila kwa uhakika zaidi tegesha sikio kwenye page yake tutatangaza kabla.
SOURCE MR PROBLEM SOLVED
Related posts
6 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/wema-azindua-kiss-lipstick/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/wema-azindua-kiss-lipstick/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/wema-azindua-kiss-lipstick/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/wema-azindua-kiss-lipstick/ […]
… [Trackback]
[…] There you will find 27156 additional Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/wema-azindua-kiss-lipstick/ […]
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/wema-azindua-kiss-lipstick/ […]