WIKI-LOVES-AFRICAin-sq-300x300Wiki Loves Africa ni shindano la picha mahususi kwa kuonyesha uzuri na utajiri wa Afrika kwa kupitia picha, sauti au video, kwa minajiri ya kutumika katika miradi mbalimbali ya Wikimedia. Shindano hili linazaminiwa na Wikimedia, na linadumu kwa muda wa miezi miwili ambalo mara zote huwa na maudhui ya aina moja kwa maana picha zote zitakazopigwa na kutumwa lazima ziwe na maudhui husika. Shindano hili kwa mwaka huu limeanza tarehe Oktoba Mosi na litaishia Novemba Thelathini. Mwaka huu maudhui yake ni Picha za Mitindo mbalimbali ya Kiafrika pamoja na Mapambo.
Chukua nafasi hii kuitangaza kazi na umahiri wako katika kupiga picha mbalimbali kwa kupiga picha za mitindo ya Nyumbani upate kuibuka kuwa mshindi wa shindano hili.
Kwa maelezo na jinsi ya kushiriki, >>>bonyeza hapa.

 

[URIS id=2068]
Chanzo: Wikipedia