MILLEN MAGESE (HAPPINESS MAGESE)
Ni miss Tanzania 2001 ambae alituwakilisha miss world mwaka huo huo 2001, baada ya kumaliza kazi zake za kuitumikia Tanzania alihamia Afrika ya kusini kuendeleza karama yake ya Uanamitindo huko alijulikana kama Millen Magesse.
Ni mwanamitindo wa kwanza kutoka Tanzania kufanya kazi na kampuni kubwa kutoka New York iitwayo FORD Pia ana fanya kazi na kampuni nyingine iitwayo Ice Model Management huko Johannesburg Afrika Ya Kusini.
Hapiness amekua kioo cha jamii kwa mengi, upendo wake, utulivu wake, uvimilivu na upiganaji wake. Hakuna kinacho mteteleza hata pale anapo kuwa na maumivu.
Amesaidia Tanzania kwa mengi kama kujenga Shule, Kuitangaza nchi yetu na pia kuwapa moyo vijana. Ametoa michango ya misaada kwenye mambo kama Tanzania Education Trust, African Rainforest Conservancy, na the MacDella Cooper Foundation.
Ameonekana kwenye majarida ya magazeti makubwa na kushirikiana na majina yenye bidhaa kubwa kama Ralph Lauren, Karen Millen, Alphadi, African Mosiaque, David Tlale, Gavin Rajah, Sun Goddess, Stoned Cherrie, Thula Sindi , Kluk CGDT, Suzanne Heynes, Heni, Clive, Laquan Smith, Tarun Talhian, Priscilla, Deola Segoe, Tiffany Amber, Korto Momulu na kadhalika . Ameonekana kwenye majarida ya magazeti kama Ladybrielle, JCK (NY), Uzuri, Bang, and Sawubona, True Love, Cosmopolitan, Elle, O Magazine, Marie Clare, Style, Glamour.
“Kutoa kitu katika jamii ni kitu ambacho nakipenda kwa sababu kinatoka moj kwa moja ndani ya moyo wangu najisikia kutimia pale nnapo weza kuwasaidia wale ambao hawana uwezo. Japo kuwa huwaga siongelei kuhusu hiyo misaada ni vizuri kuonyesha kwa matendo kuliko kuongea” amesema Hapiness.
Na juzi tu amepokea Tuzo kutoka BET Itwayo “Global Good Award” amepata tuzo hii kwa juhudi zake katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa uuitwao ENDOMETRIOSIS ambao husababisha mwanamke kuto kuzaa unao mkabili na yeye pia.
Related posts
HOT TOPICS
Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/VZ1jH2zJUg
FollowHappiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/689j7Yjcn0
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
Feza Kessy Atuelezea Kuhusu Fashion & Style Zake
Feza Tadei Kessy ni Muimbaji, Muigizaji lakini pia ni mtunzi wa nyimbo lakini pia Fezza ni former beauty queen ambapo mwaka 2005 alikuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala & Miss Tanzania Runner up. Lakini pia alishawahi kuwepo katika Reality Tv Show – Big Brother Africa. Kwa…