SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Zawadi 8 Za Kuwazawadia Wapendwa Wako Msimu Huu Wa Sikukuu Kutoka Katika Brand Za Tanzania
Mitindo

Zawadi 8 Za Kuwazawadia Wapendwa Wako Msimu Huu Wa Sikukuu Kutoka Katika Brand Za Tanzania 

Ni msimu wa kutoa nakupokea zawadi, as we all know Christmas is around na jingle bells zishaanza kulia, well wengi tunakuwa na mawazo ya nini umzawadie mpendwa wako na by mpendwa hatumaanishi tu babe ila yoyote umpendae awe mama, dada, kaka, shangazi, baba yoyote alimradi unampenda na ungependa kumpa zawadi, leo tunakuletea bidhaa 8 kutoka katika brand za ki-Tanzania ambazo sisi tumeona zinafaa kumzawadia mpendwa wako.

  • Body Spray & Perfumes 

Fyn By Falsafa – @mwanafa

 Rapper mkongwe kutoka Tanzania Hamis Mwinjuma A.K.A Mwanafalsafa au Fa amezindua bidhaa yake ambayo ni body spray aliyoipa jina la Fyn by Falsafa, well tunadhani ameitoa kipindi kizuri kabisa cha sikukuu, inauzwa shilingi elfu nne tu, kama umpendae ni mpenzi wa perfumes na spray hii zawadi nzuri ya kumpa ukizingatia it’s still hot in the market.

Aunty Body Spray – @auntyezekiel

inawezakana umekutana nayo lakini hukuwa unajua kama ni brand ya Tanzania, well yes hizi perfumes ni bidhaa kutoka Tanzania na mmiliki wake ni muigizaji maarufu Aunty Ezekiel, Tunajua mchango wa perfumes na body spray katika miili yetu, kuondoa zile jasho na karaha za harufu za hapa na pale basi Aunty Body Spray ni jibu lako.

LuvTouch Fragrance Mist / Body Splash – @shekhamanjano

Brand ya Luv Touch imetoa product mpya ambayo ni LuvTouch Fragrance Mist / Body Splash  nazo ni kwa ajili ya kujipulizia kupata harufu nzuri zipo aina tofauti tofauti inategemea na mapenzi yako, zinapatikana katika maduka ya Luv Touch kwa shilingi elfu 30,000/-

  • Beauty 

Katika mambo ya urembo, makeup, ngozi unaweza kupata bidhaa hizi kutoka kwa Tanzania pia kwa bei nafuu ambazo unaweza ku-afford

REIGN NOIR  Eyeshadow pallet – laviemakeup

Upendo Shuma au wengi tunamjua kama Lavie Makeup, amekuja na bidhaa yake iitwayo Reign Noir hii ni eyeshadow pallet huwa zinatumiwa na wanawake sana, kama una mwanadada ambae unafikiria kumpa zawadi basi hii inamfaa, kwa sasa wadada wengi wanapenda makeup add that REIGN NOIR  Eyeshadow pallet  on her makeup kit

Lavy Hand Cream – @lavyproducts

Mwanamitindo Flaviana Matata ameongeza product mpya katika kampuni yake ya Lavy Product, Product yake mpya ni hand cream kwa ajili ya kulainisha na kufanya mikono inukie, well what a gift. Unaweza mzawadia mpenzi wako REIGN NOIR  Eyeshadow pallet, Body Spray yoyote kutoka hapo juu na Lavy Hand Cream

Hii inaweza kuwa kwa upande wa kike na wa kiume

Ukili baskets by bijoux trendy – @bijouxtrendy

Unaweza kumnunulia umpandea ukili baskets kutoka kwa mbunifu Bijoux Trend anaweza kuendea sokoni, beach au hata katika maumizi ya hapa na pale ya shopping, as we all know mwaka huu ukili umetamba sana hasa hivi vikapu, na wanaweza kukuandikia chochote upendacho

Unaweza kumchukulia hii bag ya kitenge kutoka kwa mbunifu Ally Rehmtullah pia akawa anabeba kwenye mizunguko yake, hii ina bebwa na jinsia yoyote na unaonekana unadumisha vile vya nyumbani

  • Tusiwasahau watoto

Bora Star By Vanessa Mdee  – @vanessamdee

Mwanamuziki kutoka Tanzania Vanessa Mdee jana ametoa bidhaa yake ya viatu vya shule kwaa ajili ya watoto wa kike, Ikiwa wapo mapumzikoni unaweza kumnunulia mwanao viatu hivi kama zawadi ya Christmas iliaweza kuvitumia pale shule zinapofunguliwa

Well kwanini ukimbilie nje wakati vya kwetu vipo?

 

 

 

Related posts

6 Comments

  1. roof skylight

    … [Trackback]

    […] There you will find 88547 additional Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/zawadi-8-za-kuwazawadia-wapendwa-wako-msimu-huu-wa-sikukuu-kutoka-katika-brand-za-tanzania/ […]

  2. toronto weed delivery

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/zawadi-8-za-kuwazawadia-wapendwa-wako-msimu-huu-wa-sikukuu-kutoka-katika-brand-za-tanzania/ […]

  3. Bubble Tea

    … [Trackback]

    […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/zawadi-8-za-kuwazawadia-wapendwa-wako-msimu-huu-wa-sikukuu-kutoka-katika-brand-za-tanzania/ […]

  4. สล็อตเว็บตรง

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/zawadi-8-za-kuwazawadia-wapendwa-wako-msimu-huu-wa-sikukuu-kutoka-katika-brand-za-tanzania/ […]

  5. 웹툰 다시보기

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/zawadi-8-za-kuwazawadia-wapendwa-wako-msimu-huu-wa-sikukuu-kutoka-katika-brand-za-tanzania/ […]

  6. christmas jazz instrumental

    christmas jazz instrumental

    christmas jazz instrumental

Comments are closed.