SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Zuchu Anahitaji Somo La Fashion
Mitindo

Zuchu Anahitaji Somo La Fashion 

Zuchu anaweza kuwa ndiye msanii wa kike anaetamba kwasasa, speed yake katika muziki ni kubwa mno tunatamani hii speed asingeipeleka kwenye fashion pia maana anatupeleka puta in a wrong way, kwenye week moja tena week yake muhimu yote ametuvalia shaghala baghala.

Tunadhani anahitaji kukaa chini na stylist wake, amuelekeze somo la fashion kwamba fashion haihitaji mambo mengi unaweza kuvaa vitu vichache ukapendeza. Anahitaji kujua umbo lake, anahitaji kujua kimo etc.

Tumemuona kwenye hii red & gold outfit & tukawaza alikuwa ana mchannel nani? Wonder Woman au Shazam? kwanini amevaa vitu vingi namna hii? fringe jumpsuit, gold boots, blonde hair, a tiara & trench coat, Zuchu Zuchu Zuchu Zuchu, slow down this outfit looks heavy na kuna vingi vinaendelea, ambapo tunadhani angeweza kuchagua vichache akavaa. Vingi ni un-necessary mfano the trench coat, fringe kwenye jumpsuit zimeongeza uzito, the tiara unapanda jukwaani kutumbuiza unahitaji hivi vitu vyote vya nini?

well Afromates let us know your views on the below comment box.

Related posts