Tumekuwa tukipata maswali mengi kuhusu kutumia lotion ya mwilini usoni, Je ni sawa kupaka lotion ya mwili katika ngozi ya uso?

Jibu ni Hapana,

Na hii inaenda kote kwa wanaume na wanawake, wanaume wengi wanatumia lotion za mwilini kupaka na usoni pia, jua unaharibu ngozi ya uso wako bila kujua, kama lotion imeandikwa hand lotion, feet lotion, body lotion au face lotion ni vyema ikatumika sehemu usika kwa maana kuna kemikali zimewekwa zinazoendana na ngozi ya sehemu hio.