SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

NJIA ZA KUONDOA MICHIRIZI (STRETCH MARKS)
Afya

NJIA ZA KUONDOA MICHIRIZI (STRETCH MARKS) 

Stretch Marks (michirizi) hutokea sehemu mbali mbali za mwili, mikononi, miguuni, mapajani, tumboni nk, wengi hutokewa kutokana na kuongezeka kwa mwili (kunenepa) au Ujauzito hii hutokana na ngozi kutanuka. Wengi hawaipendi na wana tafuta namna ya kuziondoa unaweza kuondoa stretch marks naturally (kwa njia za asili) bila kwenda kununua madawa ya bei ghali.

1) MAFUTA YA MNYONYO

Mafuta ya mnyonyo husaidia sana kwenye ngozi kama mikunjo ya ngozi husoni, chunusi, mabaka meusi kwenye ngozi lakini pia husaidia katika kuondoa michirizi.

stretch-marks-castor-500

  • paka mafuta ya mnyonyo mahala palipo kuwa na michirizi
  • funga eneo hilo kwa mfuko wa plastic kama uonavyo pichani
  • kisha weka kitu chenye joto juu ya mfuko huo kama heating pad au chupa ya maji ya moto kwa dakika ishirini (20) kila siku mpaka utakapo ona mabadiliko.

2)ALOE VERA husifika kwa kutibu magonjwa mbali mbali ya ngozi hivyo pia husaidia kuondoa michirizi hii ya ngozi kwa njia mbili zifuatazo,

Stretch-marks500

  • kwanza unaweza kupaka Aloe Vera tu na kuiacha ikae kwenye sehemu iliyo kuwa na michirizi kwa dakika 15 kisha uoshe kwa maji ya vuguvugu au,
  • njia ya pili, ni kuchanganya majimaji ya Vitamin A, Vitamin E na Aloe Vera yenyewe kisha paka kwenye eneo lililo athirika na michirizi kila siku. Paka kama mafuta ya kupakaa mwilini.

3)SUKARI

Stretch-Marks-Sugar-Almond-Oil-Lemon-600x450

  • Chukua sukari mbichi kijiko kimoja, mafuta ya Almond na  Maji maji ya ndimu, changanya kwa pamoja halafu paka pale palipo athirika
  • Fanya hivi kila siku kabla ya kwenda kuoga, fanya kwa mwezi mzima na utaona matokeo yake.

4) JUISI YA VIAZI vina vitamini na madini ambayo kukuza ukuaji wa seli za ngozi.

Potatoes

  • kata kata kiazi chako katika vipande vyembamba
  • chukua kipande cha kiazi na ukisugue pale kwenye michirizi yako hakikisha yale maji ya viazi yame ingia kwenye michirizi ako.
  • kaa nayo kwa muda na kisha uondoe kwa maji ya uvugu vugu.

Related posts

3 Comments

  1. why is the drug molly named molly,

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/skin-care/njia-za-kuondoa-michirizi-stretch-marks/ […]

  2. สล็อตไทย

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/skin-care/njia-za-kuondoa-michirizi-stretch-marks/ […]

  3. Oregon mushroom dispensary

    … [Trackback]

    […] There you will find 41042 more Information to that Topic: afroswagga.com/skin-care/njia-za-kuondoa-michirizi-stretch-marks/ […]

Leave a Reply