Kumekuwa na maneno mengi katika uwanja wa mitindo kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu.

Wengi husema ni ngumu kwa wadau kumpa nafasi mtoto wa kike kuonyesha uwezo wake kwenye jukwaa la monyesho ya mitindo bila kuwa mahusiano nae.

IMG_0840.CR2

Jihan aliwahi kuwa Miss Tanzania (3) 2014 kwa sasa ni mwanamitindo ambaye ameonekana katika majukwaa kadhaa ya mitindo na ameweza kugusa hisia za wapenda matamasha hayo.

IMG_0841.CR2

Afroswaga haikuista kuzungumza nae juu ya kuonekana mara nyingi katika majukwaa hayo ambapo Jihan hakusita kuweka wazi na kusema “Nilivyoanza sikuwa na namjua  mtu yoyote yule, sio kweli kama ukipanda kwenye jukwaa ni lazima uwe na mahusiano. Kikubwa ni kujiamini na ukipenda kile unachokifanya, ila kama huna hivyo vitu ndio labda utaweza kufanya hayo mambo.Ila kikubwa ni ni kujituma tu na sio kusubiri kutafutiwa nafasi.

Comments

comments